×

Nature; Mkongwe anayeiendeleza Singeli

JUMA nJuma Nature

Na Andrew Carlos

JUMA Kassim Ally ‘Nature’ mmoja kati ya wanamuziki wakongwe waliofanikisha kwa kiasi kikubwa kuuweka Muziki wa Bongo Fleva katika ramani.

Nature aliyeanza rasmi muziki mwaka 1997 hadi sasa anashikilia albamu kadhaa ‘kwapani’ ambazo ni Nini Chanzo (2001), Ugali (2003), Ubinadamu-Kazi (2005), Zote History (2006) na nyinginezo.

Kwa kipindi kirefu Nature amekuwa akibadilika kwa staili za uimbaji ambapo katika nyimbo zake nyingi amekuwa akichanganya ladha tofauti za Muziki kama Hip Hop, Kwaito, Reggae na nyinginezo.

MasterJMaster Jay

Enzi hizo maprodyuza wakali kama P.Funk kutoka Bongo Records, Enrico Figueiro kutoka Sound Crafters Records, Master Jay kutoka MJ Records walikuwa wakimpatia katika kumtengenezea ‘hits’ kali na kama ukisikiliza kwa makini ngoma kama Mgambo, Inaniuma Sana, Utajiju, Sonia, Ugali utaelewa namaanisha nini.

Kwa sasa mkongwe huyo ameibuka na ngoma mpya ya Mtumba ambayo imechanganywa ladha ya Muziki wa Singeli. Kufanya kwake ngoma hiyo inaupa nguvu zaidi muziki huu wa Singeli ambao unaonekana siku zijazo kuvuka boda na kupata nembo rasmi kama muziki mkubwa kutoka Bongo.

Over Ze Weekend imepata nafasi ya kukaa chemba na Nature ambaye katika makala haya amefunguka mengi kuhusiana hasa na ujio wake huu mpya wa Mtumba.

Over Ze Weekend: Ngoma ya Mtumba ina maana gani?

Nature: Kama inavyojulikana mtumba ni neno ambalo limezoeleka kama kitu kinachodumu hivyo nilifikiria kutumia jina hilo ili kuonesha kuwa ngoma hii inadumu yaani itakaa kwa muda mrefu.

Over Ze Weekend: Idea ya Mtumba imetoka wapi?

Nature: Ukiangalia nyimbo zangu nyingi napenda kutoka kitofauti, mfano niliwahi kutoa Ngoma ya Ugali ikawa ni idea tofauti ambayo sidhani kama kuna mwanamuziki alifikiria hivyo hata na

 Mtumba ni kitu ambacho cha kipekee.

Over Ze Weekend: Vipi muziki wako kuupeleka kimataifa?

Nature: Kimataifa ndiyo mpango unaofuatia, niliamua kwanza nitoe hii ya Mtumba kama kuwaonjesha mashabiki wangu mautundu ambayo waliyamis kwa hiyo wategemee kusikia ngoma nyingine mpya na kali ambayo itakuwa ya kimataifa.

Over Ze Weekend: Unauzungumziaje Muziki wa Singeli ambao kwa sasa umeshika Bongo?

Nature: Ni muziki ambao kwa upande wangu sikuanza kuufanya leo, ni muziki unaotoka kwetu ila kwa sasa unaonekana kuendelea kutesa kama kalambwanda. Hii Mtumba ukiisikia utaona nimeamua kuweka Singeli kama sampling ndani yake hivyo bado tupo mlemle.

Over Ze Weekend: Vipi video ya Mtumba?

Nature: Video nategemea kuitengeneza Alhamisi hii na Studio ya Empty Soulz, Mwenge jijini Dar hivyo kwa sasa nipo katika mchakato wa kutafuta warembo waliopo Dar ambao watafanikisha kuwepo kwenye video hiyo na kama unajijua una sifa za kuwepo kwenye video hii nitumie picha kwa WhatsApp: 0682 878108 na baada ya hapo tutachagua na uongozi wangu wanaofaa kisha kuwatumia.

Over Ze Weekend: Unauonaje muziki wa sasa tofauti na zamani?

Nature: Muziki wa sasa mapromota wamebadilisha sana system zao. Wasanii wanaotoka ni wachache tofauti na zamani na pia kubebwa kwenye media kunachangia kwa kiasi kikubwa.

Leave a Comment