RAPA maaufu nchini Marekani, Tyga ambaye amekuwa akihusishwa na matendo ya kibui amejikuta akiingia matatani jana mara baada ya Jaji wa mahakama moja nchini humo kutaka Tyga akamatwe na aadhibiwe ikiwezekana kupewa kifungo jela ili iwe fundisho kwa wengine kutokana na kukaidi amri ya mahakama hiyo iliyomtaka afike kusikiliza kesi inayomkabili.
Tyga alitakiwa kufika mahakamani hapo jana Jumanne kujibu tuhuma zinazomkabili kuhusu kudaiwa kutolipa pesa za pango la nyumba, baada ya Tyga kukaidi agizo la mahakama, jaji aliyekuwa akiongoza kesi hiyo alivitaka vyombo vya usalama kumkamata Tyga na kumfikisha mahakamani hapo huku akiwaomba wajumbe wa baaza la mahakama wajadili adhabu ikiwezekana kumhukumu aende jela rapa huyo kutokana na dharau kubwa aliyoionesha kwa chombo hicho ch sheia kwa kutofika mahakamani hao bila kutoa taaifa yeyote.
Wakili wa mpangishaji anayemdai Tyga aliambatanisha vielelezo kuwa walikubaliana kuwa rapa angemlipa mdai wake (mwenye nyumba) kiasi cha dola milioni 16 (sawa na Tsh. milioni 3.5) kila mwezi, lakini Tyga alilipa kiasi hicho kwa miezi mitatu ya mwanzo tu, tangu wakati huo hakuwahi kulipa tena huku akiongeza kuwa, rapa huyo amezidiwa na madawa ya kulevya ndiyo yanamfanya awe na kiburi cha kutolipa deni hilo.
Kulingana na vielelezo ambavyo wakili huyto aliviwasilisha mahakamani hapo, inaonesha kuwa, Tyga aliacha kulipia pango la nyumba kwa kipindi cha takribani miaka minne sasa kuanzia Oktoba 31 mwaka 2012.
Mbali na kudaiwa pesa ya pango la nyumba, Tyga ambaye kwa sasa ameshahama kwenye nyumba hiyo anadaiwa pia pesa kwa ajili ya uharibifu alioufanaya kwenye nyumba hiyo wakati alipokuwa akiishi humo ikiwemo geti linalojiongoza lenyewe (automatic gate) na vigae vya bafuni. Vyote hivyo vinafikia gharama ya dola za Kimarekani 480,285, sawa na Tsh. bilioni 1.06.
Endapo baraza hilo la mahakama litakukaa na kuridhia kuwa Tyga afungwe jela, basi adhabu hiyo itatolewa hata kama hatofika mahakamani.