Ronaldo, aliumia goti kwenye mechi ya fainali ya Euro 2016, anaonekana kutumia muda mwingi kufanya mazoezi ya gym.
Ronaldo na Mreno mwenzake Pepe wakifanya mazoezi.
Wareno hao wkipiga picha ya pamoja kwenye uwanja wao wa mazoezi wa Valdebebas.
Cristiano Ronaldo akikaribishwa klabuni hpo na kocha wake Zinedine Zidane.
Cristiano Ronaldo na Mreno mwenzake, Pepe wamerejea Real Madrid jana Jumatano ili kukamilisha kikosi cha Mabingwa hao wa UEFA Champions ambapo kwa sasa wanajiandaa na kuanza kwa msimu mpya wa La Liga.
Wareno hao wamekuwa mapumzikoni tangu walivyotwaa ubingwa wa Uefa Euro 2016 mwezi uliopita baada ya kuichapa Ufaransa bao 1-0 dakika za nyongeza kwenye fainali ya kombe hilo.
Wote wawili waliuhusiwa kutohudhuria mechi ya juzi jumanne ambapo timu yao ya Madrid ilikuwa ikicheza na Sevilla kuwania ubingwa wa UEFA Super Cup ambapo Real Madrid walifanikiwa kutwaa kombe hilo.
UEFA Super Cup, Real Madrid Walivyoichapa Sevilla