×

Apple Kulipa Kodi Iliyokwepa Ireland

apple-inc-presentatioin-1-638

TUME ya Ulaya inatarajiwa kuiamrisha kampuni kubwa ya teknolojia ya Apple kulipa mabilioni ya dola kama kodi iliyokwepa kuilipa.

Hii inafuatia uchunguzi uliofanywa kubainisha makubaliano kuhusu kodi kati ya kampuni hiyo na Serikali ya Ireland.

Tume ya Ulaya imewalalamikia mawaziri wa Ireland kwa kuipa Apple kandarasi inayoondoa kodi kwa makubaliano ya kutoa ajira kwa raia wa nchi hiyo.

apple-icon-apple

Apple imesisitiza kwamba hakukuwa na muafaka maalum, na kwamba inalipa kodi kubwa nchini Marekani ambapo makao yake makuu yapo.

Kampuni ya Apple ni moja ya mashirika ya Marekani yanayolengwa na Tume ya Ulaya kutokana na mikataba yake ya kodi.

Leave a Comment