
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Agosti, 2016 amemteua Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Doto M.James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).
Bw. Doto M. James ataapishwa kesho tarehe 01 Septemba, 2016 saa 2:45 Asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile atapangiwa kazi nyingine.
