×

Hatimaye Aliyekuwa Rais wa Brazil Aenguliwa Rasmi Madarakani

160418_INTR_Dilma.jpg.CROP.promo-xlarge2Aliyekuwa Rais wa Brazil, Dilma Rousseff.

Rais Mpya wa Brazil, Michel Temer amesema nchi yake inaingia katika enzi mpya ya matumaini baada ya kuondoshwa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff.

Akizungumza na taifa hilo kupitia Televisheni, Rais Temer ametoa wito wa kuungana pamoja na kusema kuwa kuondolewa madarakani kwa Bi. Rousseff kumemaliza miezi kadhaa ya mashaka.

gettyimages-497374334Rais Mpya wa Brazil, Michel Temer.

Wabunge nchini humo walipiga kura ya kutokuwa na imani na Bi. Rousseff ya kumuondoa madarakani kwa asilimia 61 huku kura 20, zikipinga kuondolewa kwake.

Amekutwa na hatia ya udanganyifu wa bajeti ya nchi hiyo wakati wa kampeni zake za uchaguzi muiaska miwili iliyopita.

Brazil's President Dilma Rousseff reacts during the signing ceremony of the Civil Procedure Code at the Planalto Palace in Brasilia March 16, 2015. REUTERS/Ueslei MarcelinoMakamu wa rais , Michel Temer ambaye amemrithi Bi Rousseff kwa muda, amekula kiapo cha urais hadi ifikapo January 2019.

Katika majibu yake ya kwanza ya kura zilizopigwa, Bi Rousseff amesema kuwa, Baraza la Seneti halikutenda haki kwa mwanamke asiye na hatia.

Aidha amewashutumu Maseneta ambao walipiga kura ya kumuondoa madarakani kwamba wamehusika katika mapinduzi ya kisiasa.

Leave a Comment