×

Updates: Kutoka Rujewa Katika Kupatwa kwa Jua

kupatwa kwa jua (2) Saa 11:03 AM

Takribani theluthi moja ya jua imefunikwa na  mwezi

solar eclipse (1) solar eclipse (2) solar eclipse (3)  solar eclipse (6)  Saa 9:48 AM

Watu waambiwa wajikusanye katika makundi yenye watu 30 ili wapewe vifaa vya kutazama kupatwa kwa jua.

solar eclipse (7)Saa 9:30 AM

Mkuu wa wilaya Mbarali Reuben anawasili kwenye tukio na ulinzi usalama waimarishwa

solar eclipse (8)Saa 9:21 AM

Umati wa watu wamiminika Rujewa, Mbarali kushuhudia kupatwa kwa jua.

Rudewa (1)LEO Septemba Mosi, watalii na wanaanga kutoka mataifa mbalimbali duniani wakiwemo wanafunzi wa shule wameungana kushuhudia tukio kubwa na la kihistoria la kupatwa kwa jua katika Kata ya Rujewa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

kupatwa kwa jua (4)Ikumbukwe kuwa tukio kama hilo la kupatwa kwa jua lilitokea Julai 31,1962 takribani miaka 50 iliyopita na tukio lingine lilitokea Aprili 18, 1977, na wataalamu wa anga wanabainisha kuwa tukio kama hilo litatokea tena hapa nchini Mei 21, 2031.solar eclipse (4)

Rudewa (3)Tukio hili la kupatwa kwa jua katika eneo hilo la Kata ya Rujewa litatokea leo kuanzia majira ya saa 4:17 asubuhi ambapo eneo hilo litaonekana kwa asilimia 90 hadi umbali wa kipenyo cha kilometa 100.

Rudewa (2)Serikali ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambayo itakuwa mwenyeji katika kushudia tukio kubwa na la kihistoria la kupatwa kwa jua, imewahakikishia ulinzi na usalama wa kutosha wageni wote watakaojumuika leo kushuhudia tukio hilo.

Rudewa (2)Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune anaeleza kuwa ni umbali wa Kilometa 3.5 kutoka Barabara kuu ya Iringa hadi Mbeya ili kulifikia eneo hili lililopendekezwa na wana anga kuwa mahali sahihi pakushuhudia tukio hilo.

Rudewa (1)Ili kuweza kutazama tukio hilo la kupatwa kwa jua kwa uzuri zaidi wataalamu wa anga wameeleza kuwa tayari wamefanya maandalizi ya vifaa maalumu kwa ajili ya tukio hilo.kupatwa kwa jua (3)

Leave a Comment