Hivi karibuni imethibitika kuwa staa wa muziki nchini Nigeria, Wizkid anatoka kimahaba na rafiki wa karibu wa familia ya Kardashian aitwaye Justin Skye.
Wiz alithibitisha mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka picha ya mrembo huyo na kuandika maneno yanayoashiria kabisa moja kwa moja kuwa wanatoka kimahaba.
Justin Skye na wadogo zake na Kim Kardashian.
Justin Skye ni rafiki wa karibu sana na mdogo wake na Kim Kardashian, Kylie Jenner (wa chini kulia kwenye picha hapo juu).
Staa huyo wa Naija hip hop ambaye kwa sasa ana watoto wawili, mmoja akiwa amezaa na mwanamke wa Kinigeria na mwingine aliyempata hivi karibuni aliyekuwa mpenzi wake wa Amerika, Binta Diamond Diallo inasemekana anatarajia kupata mtoto wa tatu kupitia kwa mpenzi wake huyo mpya Justin Skye.

