Nyumba hiyo ndogo yenye jina la Ufalme wa Dhahabu.
Athumani akiingia ndani ya nyumba hiyo.
Athumani akionesha baadhi ya picha za wanyama alizozichora.
….akiwa ndani ya nyumba hiyo.
NA DENIS MTIMA/GPL
VIJANA wa Kitanzania; Athumani Kilumamula na Malick Gumbizi, wameonesha ubunifu wa ajabu unaosababisha kuwavutia watu wengi wanaopita katika barabara ya Morogoro eneo la Manzese-Argentina jijini Dar.
Ukifika maskani kwao utakutana na nyumba ndogo waliyoibuni yenye maandishi yanayosomeka ‘Jumba la Ufalme wa Ajabu’ ambayo imenakshiwa na rangi ya dhahabu.
Mtandao huu uliangaza eneo hilo na kuzungumza na Athumani ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Hapa mimi nafanya kazi ya ubunifu huu nikiwa na mwenzangu aitwaye Malick Gumbizi wote sisi ni wakazi wa Manzese, shughuli hii ya ubunifu wa vitu mbalimbali na uchoraji ndiyo inatufanya kuishi hapa mjini kwani tunapopata mteja wa kumbunia kitu na kumtengenezea tayari tunakuwa tumejiingizia kipato na familia zetu kwa ujumla.”
Alisema katika shughuli hiyo, wanachotumia ni rangi, mbao, misumari na nyundo kwa ajili ya kupigilia misumari. Mbali na hilo, Athumani alisema pia wanajihusisha na masuala ya kuchora michoro ya vitu vya asili na kuprint fulana za aina yoyote lakini changamoto kubwa waliyonayo ni eneo hilo kutokuwa rafiki kibiashara licha ya kuwa watu wengi wanaona na kuvutiwa na kazi zao.
Alifafanua kuwa katika sanamu ya mchoro unaoonekana katika picha wametumia mbao za ‘ceiling board’, maboksi na rangi ya dhahabu kwa ajili ya urembo hivyo kwa mteja atakayevutiwa na kazi zao anaweza kuwasiliana nao kwa namba: +255 652 175752 au +255 773 530714.



