Msanii wa Singeli aitwaye Dogo Nigga akiwarusha vilivyo wakazi wa Tabata Dar katika tamasha hilo.
Mmoja wa wasikilizaji wa radio Efm akishindqa kujizuia na kuonekana akiserebuka vilivyo.Wasikilizaji wa Efm wakiendelea kuburudika.Msanii wa Singeli aitwaye Dogo Nigga akiwarusha vilivyo wakazi wa Tabata Dar katika tamasha hilo.
Wasikilizaji wa Efm wakiendelea kuburudika.
KITUO cha Redio cha Efm kilichopo Kawe-Mikocheni jijini Dar, chini ya udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom usiku wa kuamkia Jumapili ya Septemba 18 mwaka huu ilitua Wilaya ya Ilala katika Baa ya Toroka Uje iliyopo Tabata na kusepa na kijiji katika tamasha lao lijulikano kama Muziki Mnene.
Katika tamasha hilo, burudani ilikuwa ya aina yake na shangwe kila kona kutoka kwa mashabiki waliofurika katika baa hiyo pale walipokuwa wakipanda wasanii wanaokuja kwa kasi kupitia muziki wa Singeli.
Lengo la tamasha hilo ni kukutana na kuwashukuru wasikilizaji wao katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar na Mkoa wa Pwani, kwa namna walivyoipokea Efm Radio na kushirikiana nao hadi kufikia sasa.
Akizungumza na mtandao huu Meneja wa Efm, Dennis Ssebo, alisema tamasha la Muziki Mnene mwaka huu linafanyika kwa kipindi cha muda wa miezi mitatu ambapo muziki unapigwa katika baa 12 za jiji la Dar na Pwani likiwa limebeba kauli mbiu ya ”TUNASEPA NA KIJIJI” ikiwa na maana kuwa, kila wiki Efm inaweka kambi katika kijiji kimoja ama eneo moja kwa muda wa siku nne.
Aidha muziki mnene eneo husika unapokuwa umetua huenda sanjari na kampeni ijulikanayo ‘NJE NDANI’ ambapo vipindi vinne vinarushwa moja kwa moja (live) katika mtaa husika ambavyo ni Uhondo (Siku ya Jumatano), Sports Headquarters (Alhamisi), Joto la Asubuhi (Ijumaa) pamoja na Funga Mtaa (Jumamosi) na burudani kutoka kwa RDJ’s Mamy wa Efm.
Pia kwa muda wa asubuhi, Muziki Mnene unapokuwa umetua panakuwa na Jogging, Muziki wa Singeli, michano kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki ambapo anayeibuka mshindi hupewa fursa ya kupigiwa nyimbo zake kupitia radio hiyo na mpira wa miguu kati ya timu ya Efm na timu za Maveterans wa eneo husika.
Na Hilaly Daud/Gpl