
Wiki kadhaa, staa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alizua gumzo kubwa baada ya kuchaguliwa kuwania Tuzo za BET 2021.
Baadhi ya watu waliandamana kutokumpigia kura kwa madai kwamba Diamond au Mondi anafungamana na tabaka tawala ambalo kwao linaonekana kukandamiza tabaka la chini.
Katika tuzo hizo, Mondi anawania Kipengele cha Best International Act na sasa yupo kwenye dakika za lala salama kwa sababu shughuli yenyewe ni Jumapili hii ya Juni 28 huko nchini Marekani.
Mondi anashindana na wakali wengine kama Aya Nakamuraa (Ufaransa), Burna Boy (Nigeria), Emicida (Brazil), Headie One (Uingereza), Wizkidayo (Nigeria), YoungTand Bugsey (Uingereza) na Youssouphamusik (Ufaransa).

Aidha, katika mitandao ya kijamii hasa Twitter baadhi ya watumiaji walionekana kutofurahishwa na Mondi kuchaguliwa kuwania tuzo hizo hivyo walidhamiria kuwapigia kura wasanii wengine kutoka mataifa mengine hasa Nigeria.
Hata hivyo, IJUMAA linafahamu kwamba hakukuwa na nafasi ya mashabiki kupiga kura bali kura zinapigwa na akademi maalum ya BET yenye watu 50.
Mondi ambaye mara kadhaa amekuwa akionekana kwenye majukwaa mbalimbali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa kwenye kampeni, alikabiliwa na shutuma kutoka kwa baadhi ya watumiaji wa Mtandao wa twitter kwamba anashirikiana na chama kinachounda Serikali ambayo ilionekana ni kandamizi kwa wananchi hao.
Aidha, baadhi ya watumiaji hao walikosoa kitendo hicho na kusema si cha kizalendo huku wakiunga mkono na kuahidi kuwa pamoja naye bega kwa bega.
Imekuwa ni dhana ya wasanii wengi duniani kote kujitokeza na kuingia kwenye siasa kama wagombea mfano, MwanaFA, Bobi wine, Profesa Jay, Wakazi, Sugu na wengine wengi.
Pia, wapo wasanii wengi hupanda katika majukwaa mbalimbali ya siasa kutumbuiza kipindi cha kampeni kama afanyavyo Mondi kama Stamina, Maua Sama, Rayvanny, Young Killer, King Kiba, Mr Blue, Harmonize na wengine wengi.
ALBUM OF THE YEAR
- After Hours – The Weeknd
- Blame it on Baby – DaBaby
- Good News – Megan Thee Stallion
- Heaux Tales – Jazmine Sullivan
- King’s Disease – Nas
- Ungodly Hour – Chloe x Halle
BEST COLLABORATION
- “WAP” – Cardi B feat. Megan Thee Stallion
- “Rockstar” – DaBaby feat. Roddy Ricch
- “Popstar” – DJ Khaled feat. Drake
- “Whats Poppin (Remix)” – Jack Harlow feat. DaBaby, Tory Lanez & Lil Wayne
- “Cry Baby” – Megan Thee Stallion feat. DaBaby
- “For the Night” – Pop Smoke feat. Lil Baby & DaBaby
BEST FEMALE R&B / POP ARTIST
- Beyoncé
- H.E.R.
- Jazmine Sullivan
- Jhené Aiko
- Summer Walker
- SZA
BEST MALE R&B / POP ARTIST
- 6LACK
- Anderson .Paak
- Chris Brown
- Giveon
- Tank
- The Weeknd
BEST NEW ARTIST
- Coi Leray
- Flo Milli
- Giveon
- Jack Harlow
- Latto
- Pooh Shiesty
BEST GROUP
- 21 Savage & Metro Boomin
- Chloe x Halle
- Chris Brown & Young Thug
- City Girls
- Migos
- Silk Sonic
BEST FEMALE HIP HOP ARTIST
- Cardi B
- Coi Leray
- Doja Cat
- Megan Thee Stallion
- Latto
- Saweetie
BEST MALE HIP HOP ARTIST
- DaBaby
- Drake
- J. Cole
- Jack Harlow
- Lil Baby
- Pop Smoke
BOBBY JONES BEST GOSPEL/INSPIRATIONAL AWARD
- “In Jesus Name” – Bebe Winans
- “Never Lost” – Cece Winans
- “Hold Us Together” – H.E.R.
- “Strong God” – Kirk Franklin
- “Thank You for It All” – Marvin Sapp
- “Touch From You” – Tamela Mann
BET HER AWARD
- “So Done” – Alicia Keys Ft. Khalid
- “Baby Mama” – Brandy feat. Chance the Rapper
- “Anti Queen” – Bri Steves
- “Baby Girl” – Chloe x Halle
- “Rooted” – Ciara feat. Ester Dean
- “Good Days” – SZA
BEST INTERNATIONAL ACT
- Aya Nakamura (France)
- Burna Boy (Nigeria)
- Diamond Platnumz (Tanzania)
- Emicida (Brazil)
- Headie One (UK)
- Wizkid (Nigeria)
- Young T & Bugsey (UK)
- Youssoupha (France)
VIEWER’S CHOICE AWARD
- “WAP” – Cardi B feat. Megan Thee Stallion
- “Go Crazy” – Chris Brown & Young Thug
- “Rockstar” – DaBaby feat. Roddy Ricch
- “Popstar” – DJ Khaled feat. Drake
- “Laugh Now Cry Later” – Drake feat. Lil Durk
- “The Bigger Picture” – Lil Baby
- “Savage (Remix)” – Megan Thee Stallion feat. Beyoncé
- “Leave the Door Open” – Silk Sonic
VIDEO OF THE YEAR
- “Up” – Cardi B
- “WAP” – Cardi B feat. Megan Thee Stallion
- “Do It” – Chloe x Halle
- “Go Crazy” – Chris Brown & Young Thug
- “Laugh Now Cry Later” – Drake feat. Lil Durk
- “Leave the Door Open” – Silk Sonic
VIDEO DIRECTOR OF THE YEAR
- Benny Boom
- Bruno Mars and Florent Déchard
- Cole Bennett
- Colin Tilley
- Dave Meyers
- Hype Williams
BEST MOVIE
- Coming 2 America
- Judas and the Black Messiah
- Ma Rainey’s Black Bottom
- One Night in Miami…
- Soul
- The United States vs. Billie Holiday
BEST ACTRESS
- Andra Day
- Angela Bassett
- Issa Rae
- Jurnee Smollett
- Viola Davis
- Zendaya
BEST ACTOR
- Aldis Hodge
- Chadwick Boseman
- Damson Idris
- Daniel Kaluuya
- Eddie Murphy
- Lakeith Stanfield
YOUNGSTARS AWARD
- Alex R. Hibbert
- Ethan Hutchison
- Lonnie Chavis
- Marsai Martin
- Michael Epps
- Storm Reid
SPORTSWOMAN OF THE YEAR AWARD
- A’ja Wilson
- Candace Parker
- Claressa Shields
- Naomi Osaka
- Serena Williams
- Skylar Diggins-Smith
SPORTSMAN OF THE YEAR AWARD
- Kyrie Irving
- LeBron James
- Patrick Mahomes
- Russell Westbrook
- Russell Wilson
- Stephen Curry
Stori; Sifael Paul, Dad