×

Wanamitindo Kuchangia Vita Dhidi Ya Saratani Ya Matiti

saratani-zenji-2-001saratani-zenji-3-001 saratani-zenji-4-001 saratani-zenji-5-001…Ni majaji hao wakiwasikiliza kwa makini wanamitindo (hawapo pichani)  wakijibu maswali.

saratani-zenji-6-001Baadhi ya wanamitindo wakijibu maswali.

saratani-zenji-1-001Wanamitindo wakiwa katika picha ya pamoja na majaji.

Wanamitindo kutoka  kampuni ya  mitindo ya Black Fox  ya Msasani jijini Dar, jana walikuwa katika mazoezi ya mwisho  kujiandaa na maonesho ya  mavazi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 8, katika Ukumbi wa  Zanzibar Grand Palace,  visiwani  Unguja,  kwa ajili ya uchangishaji wa kusaidia wagonjwa wa saratani ya matiti waliyoyapa jina ya Marashi ya Pwani.

 Wanamitindo hao jana walikuwa katika mchuoano wa mwisho  ili   kuwapata wanaoweza kuwa mabalozi wenye uelewa stahiki wa ugonjwa huo watakaowaeleza watu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo na  kukabiliana nao pindi mtu  anapoupata.

Majaji  watakaoendesha shughuli siku ya hafla hiyo hiyo  ambao ni Kulwa Nkwandule (wa kwanza kulia)  ambaye ni mmoja wa waandaji , Nadia Azmat (katikati)  ambaye ni mdhamini mkuu na wa mwisho ni Aj Myner.

Na Imelda Mtema.