Dar es Salaam: Mazishi ya bondia Thomas Mashali aliyeuwawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana yanatarajia kufanyika kesho Jumatano, Novemba 2, 2016 katika makaburi ya Kinondoni yaliyopo jijini Dar es Salaam.Baba mzazi wa Mashali amesema wameamua kufanya mazishi hayo Jumatano kwa kuwa wanapisha uchunguzi wa polisi.
“Tumewaachia kidogo polisi wamalizie kazi yao, lakini mazishi yatakuwa Jumatano badala ya Jumanne kama ilivyokuwa hapo awali,” alisema.
Msiba wa bondia huyo ambaye ameuwawa na watu wasiojulikana uko kwao Tandale jijini Dar es Salaam.
Kama ulikosa video ya Baba Mzazi wa Bondia Thomas Mashali Akiongelea kwa uchungu Kifo cha Mwanaye