×

Mourinho Amrudisha Schweinsteiger, Luke Shaw Amtabilia Makubwa Kikosini

jose_mourinho_was_on_hand_to_cas

MANCHESTER: Hatimaye kiungo Bastian Schweinsteiger amerejea kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Man United baada ya kufanya mazoezi mwenyewe au na kikosi cha chini miaka 23 kwa muda wa miezi miwili.

united_captain_wayne_rooneyNahodha huyo wa zamani wa Ujerumani kwa mara ya mwisho aliichezea Man U mwezi Machi wakati Louis van Gaal alipokuwa kocha wa mashetani hao wekundu.

Alisema mwezi August kuwa hana tatizo binafsi na Mourinho na Man U itakuwa klabu yake ya mwisho kucheza barani Ulaya.

schwescteigerKwa upande wake, mchezaji wa Manchester United, Luke Shaw amemtabilia makubwa Mjerumani huyo na kusema kuwa kwa sasa Mashetani Wekundu hao watakuwa na performance nzuri zaidi baada ya kurejea kikosini Schweinsteiger aliyekuwa ametoswa na Mourinho.

luke-shaw-na-schwensteigerSchweinsteiger ambaye ameisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Dunia mwaka juzi 2014 na Champions League, amejikuta akiwa kama uhamishoni vile baada ya ujio wa Mourinho Man U aliyemtema kikosini na kusema kuwa hataki kumtumia wala kumuona mazoezini kikosini hapo. Lakini jana ilikuwa tofauti baada ya mkali huiyo kurejea kikosini tena na kuleta matumaini kwa staa huyo na mashabiki wa Man U.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya soka wanadai kuwa, Morinho amemrudisha Schweinsteiger aidha kutokana mwendelezo wa matokeo mabaya wanayoyapata kwenye mechi zao au ni kwa sababu ya Ander Herera kupigwa kadi nyekundu kwenye mechi yao dhidi ya Burnley iliyopigwa wiki jana nyumbani kwao Old Traford ambapo Man U alitoa droo ya 0-0.