×

UEFA: Arsenal Wanusurika, Waichapa Ludogorets Razgrad 3-2 Dakika ya 87

ozil-1 Mesut Ozil alifunga bao la dakika za lala salama na kuwawezesha Arsenal kutoka nyuma ambapo mwanzoni walikuwa wamepigwa 2-0 na hatimaye kuilaza Ludogorets Razgrad ya Bulgaria 3-2 na kuwafikisha hatua ya mtoano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

ozil-2Ozil alionekana kutulia alipokimbia langoni, akampiga chenga kipa na mabeki wawili na kisha akatumbukiza mpira kimiani.

Awali, matumaini ya Arsenal kurudia ushindi wao mkubwa wa 6-0 mechi ya kwanza yalizimwa Jonathan Cafu alipowaweka Ludogorets mbele baada ya frikiki ya Wanderson.

arsenal-1 Cafu alisaidia ufungaji wa pili alipomzidi ujanja Kieran Gibbs na kumpa mpira Claudiu Keseru aliyefunga na kuwashangaza Arsenal.

Granit Xhaka aliokoa jahazi upande wa Arsenal kwa kombora la kutoka hatua 15 kutoka kwa goli baada ya kupokea krosi kutoka Ozil na kufufua matumaini ya Arsenal kwa bao moja.

arsenal-2Olivier Giroud naye alifunga kwa kichwa kutoka kwa mpira uliotoka kwa Aaron Ramsey na kusawazisha.

Kipa wa Arsenal David Ospina alifanya kazi ya ziada kuokoa mpira mara mbili kutoka kwa Wanderson kabla ya Ozil kufunga.

_92218416_groupaArsenal sasa wamefika hatua ya 16 bora na wameendeleza msururu wao wa kutoshindwa hadi mechi 15.

MATOKEO Kamili: Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya

KUNDI A

Basel 1-2 Paris Saint Germain

Ludo Razgd 2-3 Arsenal

KUNDI B

Besiktas 1-1 Napoli

Benfica 1-0 Dynamo Kiev

KUNDI C

Bor Monchengladbach 1-1 Celtic

Manchester City 3-1 Barcelona

KUNDI D

Atletico Madrid 2-1 FC Rostov

PSV Eindhoven 1-2 Bayern Munich

Video ya Magoli Yote