×

Olive Kiarie Mshindi wa Mil. 30 Za Maisha Plus East Africa 2016

winner

maisha-plus-6Mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016 kutoka Kenya, Olive Kiarie (aliyekaa)  baada ya kutangazwa.

maisha-plus-8 maisha-plus-7…Akipongezwa na washiriki wenzake.

maisha-plus-11

…Akikabidhiwa zawadi yake na hundi ya Tshs. Milioni 30.

maisha-plus-10

Pongezi zikiendelea.

maisha-plus-5

Mwakilishi kutoka Azam Media akimtangaza mshindi.

maisha-plus-13

Baadhi ya washiriki  kutoka Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.  Aliyekaa kwenye ndoo ni kiongozi wa kambi ya Maisha Plus aitwaye Babu.

maisha-plus-14

Kiongozi Mtendaji wa kampuni ya DMB (waandaaji wa Maisha Plus), Masoud Ali ‘Masoud Kipanya’ (kushoto) akiongea na staa  wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz.

maisha-plus-1

Msanii wa Bongo Fleva kutoka kundi la Weusi, John Makini (kulia), akiongea na Masoud.

maisha-plus-2

Washiriki waliotinga tano bora ya Maisha Plus East Africa 2016.

maisha-plus-3

Waliotinga tatu bora.

Mshiriki kutoka Kenya, Olive Kiarie, ameibuka mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016 na kujishindia kitita cha Tzshs. Milioni 30.

Alichosema baada ya kushinda:  “Kwanza napenda kumshukuru Mungu. Nimetoka Kenya kuja kutafuta hii pesa na nimeipata, hivyo namshukuru Mungu. Nawashukuru marafiki zangu wote walionipa sapoti. Asante pia Babu.”   Olive aliyasema hayo huku akitoka machozi.

Hii ni mara ya kwanza kwa taji hilo kwenda nje ya Tanzania ikiwa ni msimu wa tano toka mashindano haya yaanze mwaka 2009. Olive anakuwa msichana wa pili kujishindia taji hilo baada ya Bernick Kimiro aliyeshinda mwaka 2012.

Shindano la Maisha Plus lilijumuisha washiriki 30 kutoka nchi tano za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda ambapo washiriki 16 tu ndiyo waliofanikiwa kuingia fainali. Washiriki Aloyce Sambuta, Irene Ishengoma, Alex Essau, Ngenda Pilly, Nibigira Baswari, Grace Pemba, Denaice Machocho, Umubyeyi Solange, Assimwe Marvin, Salmin Omary, Rukia Athuman, Mike Curtywer, Yasinta Mrisho, Karekezi Jean na Namita Cherrie walifanikiwa kuingia fainali ambazo zilirushwa jana usiku na kituo cha televisheni cha Azam Two.