×

Rais JPM Atumia Saa 2 Kutathimini Mwaka Mmoja Madarakani na Wanahabari

rais-na-wanahabari-9 rais-na-wanahabari-10

rais-na-wanahabari-8

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

  rais-na-wanahabari-3 rais-na-wanahabari-5

Wanamuziki Mrisho Mpoto na Banana Zorro wakitoa burudani wakati wa mkutano wa Rais Magufuli na wanahabari leo.

rais-na-wanahabari-6 rais-na-wanahabari-7  

Sehemu ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Rais Magufuli.

rais-na-wanahabari-12

Wanahabari kutoka Global Publishers Ltd wakifuatilia mkutano huo.

rais-na-wanahabari-11

 rais-na-wanahabari-13 rais-na-wanahabari-14

Mwanamuziki Mrisho Mpoto akitoa burudani mbele ya Rais Magufuli.

rais-na-wanahabari-15

Rais Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanahabari baada ya mkutano huo.

rais-na-wanahabari-16 rais-na-wanahabari-17 rais-na-wanahabari-18

Rais Dk. John Pombe Magufuli (katikati waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (wa pili kulia waliokaa), Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media Ltd Tido Mhando (wa tatu kulia waliokaa) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Rioba (wa tatu kushoto waliokaa) pamoja na wanahabari kutoka vyomba mbalimbali vya habari. 

DAR ES SALAAM: RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, leo amekutana na wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari na kutoa tathimini yake ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani.

Rais alikutana na wanahabari hao, Ikulu jijini Dar ambapo alitumia saa 2 na dakika 45 kujibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na wahariri waliokusanyika katika moja ya kumbi zilizopo Ikulu.

Awali, alianza alipoulizwa na wanahabari kuhusu tathimini yake ya mwaka mmoja madarakani, alisema ni vyema watu wakamtathimini zaidi kuliko yeye kujitathimini kulingana na yale aliyoyaahidi kupitia ilani ya chama chake cha Mapinduzi.

Hata hivyo, rais alisema kwa ujumla anauona mwaka mmoja alioutumia madarakani, unatosha kumpa picha ya Tanzania anayoitaka kwani kupitia bajeti ya mwaka 2016/2017 iliyopitishwa bungeni, inajidhihirisha ni jinsi gani serikali yake imedhamiria kupiga hatua hususan katika miradi ya maendeleo ambayo bajeti yake ameipa asilimia 40 tofauti na asilimia 26 za bajeti ya mwaka jana.

“Ukiangalia kwa mfano tu bajeti ya miundombinu, tumetenga Trilion 4.7. Zaidi ya Trilion 1 imetengwa kwenye reli ambapo ujenzi wa awamu ya kwanza utaanza Dar mpaka Morogoro. Tumeagiza ndege mbili mpya aina ya Bombardier Dash8 Q400, tumeagiza nyingine mbili na tunategemea mpaka kufikia mwaka 2018, ndege takriban saba zitakuwa zimeingia nchini kwa ajili ya kurahisisha usafiri ili kusudi hata watalii wetu wawe wanatoka kwao moja kwamoja hadi nchini,” alisema Magufuli.

Kama hiyo haitoshi, rais Magufuli alitumia nafasi hiyo kueleza mambo mbalimbali ambayo yamekuwa ni changamoto kwa serikali yake ikiwemo suala la watumishi hewa, rushwa ambapo alisema tayari ameshachukua hatua stahiki sambamba na kurejesha nidhamu kwa watumishi wa serikali.

Pia alizungumzia mahakama ya mafisadi, akasema tayari ameshasaini sheria ya mahakama maalum ya kushughulikia mafisadi na tayari imeanza kufanya kazi tangu jana ambapo kesi ya kwanza imeanza kusikilizwa.
Aidha, Rais Magufuli aliizungumzia ‘Tanzania ya Viwanda’ kwa kusema jukumu lao kama serikali ni kuwezesha sekta binafsi na serikali yenyewe kuwa na viwanda na hilo tayari limeshaanza kuonekana kupitia viwanda mbalimbali ambavyo vimeanza kutoa ajira.

Akifafanua kuhusu suala la kutoa ajira serikalini, Rais Magufuli alisema Watanzania wanapaswa kutambua kwamba, alisimamisha zoezi la kutoa ajira kwa kipindi cha miezi miwili ili kufanya uhakiki wa watumishi hewa, zoezi ambalo hadi sasa wanaendelea nalo lakini ajira tayari serikali imeanza kutoa.

“Tulibaini zaidi ya watumishi hewa elfu kumi na saba. Na bado uhakiki unaendelea huenda wakafika hata elfu ishirini,” alisema Magufuli.

Mbali na hayo, rais pia alizungumzia changamoto mbalimbali ikiwemo suala la mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo pia walibaini baadhi ya wanafunzi walikuwa ni hewa na kuna wanafunzi wengi ambao walikuwa wakichukua mikopo pasipo kuirejesha.

Habari / Picha: Erick Evarist na Clarence Mulisa / GPL