Jopo la wadhamani na waandaaji wa tuzo hiyo wakiwa kwa pamoja.
Katibu mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania Godfrey Mungereza akizungumza jambo.
Muakilishi kutoka kampuni ya Coca Cola ambaye ni mmoja wa dhamini Anna Lugenge akizungumza jambo.
Mmoja waandaji wa tuzo hizo kutoka EATV,Loy akimkabidhi mmoja wa wawaklisha kutoka Vodacom Ibrahim Kaude karatasi ya majina ya wasanii walioingia kwenye kinyanganyiro hicho.
Tuzo zinazowania kupitia televisheni ya East Afrika zimeanza kunukia baada ya washiriki wengine walioingia katika kinyan’ganyiro hicho zenye vipengele kumi zimetajwa ambapo nia na madhumuni ni kuwatunza wasanii wa filamu na muziki ambao wamejipendekeza wenyewe kwa kujaza fomu maalum.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Sleep Way iliyopo Masaki jijini Dar, mratibu wa shidano hili Roy, alisema kuwa tuzo hizo zinatarajia kufanyika tarehe 10 Desemba,katika ukumbi wa Mlimani City ambapo wasanii tisa na tunzo moja ya heshima zitatolewa.