RAIS Muhammadu Buhari wa Nigeria ametakiwa kuachia nafasi hiyo na kundi la upinzani la vyombo vya habari linalojulikana kama Wailing Wailers.
Wito huo ulitolewa na Wailing Wailers katika mtandao wa Twitter kulingana na taarifa yake iliyosainiwa na katibu wake wa kitakfa, Usman Abubakar, ambayo inasema hapana mafanikio yoyote yaliyopatikana chini ya Rais Buhari tangu kuapishwa kwake Mei 25 mwaka 2015.
Wito huo wa kujiuzulu Buhari umeibuliwa na harakati kubwa zinazofanywa na mitando ya vijana nchini Nigeria kuhusiana na masuala ya kijamii.
Kampeni mpya iliyoanzishwa imepewa jina la #BuhariMustGo



