×

Menejimenti ya Shirika la Ndege Tanzania Yavunjwa

atcl

DAR ES SALAAM: Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeivunja Menejimenti ya Shirika hilo ili kukidhi vigezo na haja za Shirika hilo na malengo yaliyowekwa kwa miezi nane huku ikiamuru wakurugenzi wotena baadhi ya mameneja waondolewe mara moja isipokuwa mtendaji wake mkuu aliyeajiriwa hivi karibuni.

Hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo utendaji dhaifu, viwango hafifu vya elimu kinyume na matakwa ya nafasi hizo na uadilifu wakati wakurugenzi na Mameneja waliokuwa wakikaimu nafasi mbalimbali imeamriwa warudishwe kwenye ngazi zao za chini.

Bodi imemuagiza Mtendaji Mkuu atangaze nafasi za Wakurugenzi, Mameneja na nafasi nyingine atakazoona zinafaa kutafutiwa wafanyakazi wapya.

Pia bodi hiyo imesema wamepunguza sana matumizi yasiyo ya lazima na wana mpango wa kuongeza safari za ndani za Kilimanjaro na Mtwara, pia wamefanikiwa kuongeza mapato ya ndani yatokanayo na mizigo iliyozidi, wanadhibiti utolewaji wa tiketi za bure unaotolewa kwa wafanyakazi wa shirika ambao unaonekana kutumiwa vibaya na wafanyakazi.

Hata hivyo hatua zaidi zitachukuliwa kwa mawakala wa kukatisha tiketi kwakuwa utaratibu uliokuwepo hakuangalia maslahi ya shirika na ikithibitika hakuna ulazima wa kuwatumia mawakala basi kutakuwa na zoezi la kubatilisha mikataba ya mawakala na kuwatumia wafanyakazi wa Shirika.

Mwenyekiti wa bodi ATCL amedai shirika lilikuwa linakopa sana zamani na sasa wachofanya ni kulipa madeni ya zamani.

Pia amesema wamejitahidi kutatua changamoto mbalimbali kama ucheweshaji wa ndege na wanaendelea kutatua changamoto ya uhaba wa marubani ambapo hadi sasa marubani wanne wamemaliza mafunzo na wengine wanne wanatarajia kumaliza mafunzo mwishoni mwa mwezi huu mafunzo hayo yanacchukua muda kwa kuwa yanategemea ndege mpya mbili tu.

Awamu ya mwisho ya ukamilishaji wa mafunzo inatarajiwa kumalizika mwezi Disemaba ambapo itaifanya ATCL kuwa na marubani 13.

Baada ya kuanza safari zake Octoba 14 2016,Shirika la Ndege la ATCL limekili kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo ucheleweshaji wa ndege na kutoa huduma katika maeneo ambayo yalipaswa kuhudumiwa.

Akitoa changamoto hizo, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Mhandisi Emmanuel Korosso amekili kuwepo kwa changamoto ya Marubani katika Shirika hilo ikizingatiwa mpaka sasa Shirika hilo linatarajiwa kumaliza mafunzo ya Marubani 13 katikati ya mwezi Desemba.

Amesema kuhusu Wafanyakazi Bodi yake imeagiza Menejimenti ya Shirika kusimamisha kwa muda mkataba wa hiari ambao unatoa mwanya kwa wafanyakazi kutumia vibaya ruhusa za matumizi ya tiketi za bure.

“Katokana na haja ya kuboresha Utendaji, ATCL iliamuliwa Wakurugenzi wote katika Menejimenti ya ATCL isipokuwa Mkurugenzi Mtendaji, na baadhi ya Menejimenti waondolewe katika nafasi zao Mara moja kutokana na Utendaji dhaifu na viwango vya Elimu visivyokidhi matakwa ya nafasi zao”,amesema Mhandisi Korosso

“Tumeamua wakurugenzi wanaokaimu nafasi zao warudishwe katika nafasi zao za chini ambazo siyo za Menejimenti au wahamishiwe katika vituo vya mikoani”,ameeleza Mhandisi Korosso

Aidha, Wakurugenzi na Menejimenti waliokuwa wamethibitishwa tumeagiza waondolewe ATCL ili wapangiwe majukumu mengine kulingana na sifa zao.

Aidha Bodi imemuagiza Mtendaji Mkuu kutangaza mara moja nafasi zote za Wakurugenzi na pia nafasi za Mameneja zilizo wazi kwa kufuata muundo wa muda uliopitishwa na Bodi (Interim Organization Structure).

Pia Mtendaji Mkuu ameagizwa kutangaza nafasi zozote ambazo anaona kuna umuhimu wa kuajiri watu wengine kutokana na utendaji usioridhisha wa wafanyakazi wanaoshikiria nafasi hizo kwa sasa.

halotel-strip-1

 Makonda Alivyobaini Uchafu wa Soko la Samaki Feri Unavyoasiri Mapato ya Nchi