DAR ES SALAAM: HAYAWI HAYAWI YAMEKUWA; Kocha mpya wa Klabu ya Yanga, George Lwandamina ametua kikosini hapo na kukabidhiwa jukumu la kuinoa klabu hiyo akichukua nafasi ya Mholanzi, Hans Van der Pluijm aliyepewa jukumu la kuwa Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi.
Makamu wa Rais wa Yanga, Clement Sanga (katikati) akimtambulisha kocha lwandamina kwa wanahabari.
Awali Yanga hawakutaka kumzungumzia kocha huyo. Baada ya kutambulishwa rasmi, Kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina amesema atapambana vilivyo kuhakikisha anafanya vema.
Hans van der Pluijm akizungumza na wanahabari.
Lwandamina akijibu maswali ya wanahabari.
Lwandamina ameomba Wanayanga kumpa ushirikiano ili kufikia malengo yake. Lakini amesisitiza suala la ushrikiano ni namba moja kwake.
MWANAFUNZI APIGWA RISASI NA POLISI DAR ES SALAAM……



