KOCHA Mkuu mpya wa Yanga, raia wa Tunisia, Mohammed Nabi, juzi jioni alianza kibarua cha kukinoa kikosi hicho akitumia saa moja kuwapa mazoezi ya kimbinu kwa kuanzia safu ya ulinzi na ushambuliaji pekee.
Mtunisia huyo alianza kibarua hicho juzi Alhamisi saa kumi kamili kwenye Uwanja wa Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ilipoweka kambi Yanga ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho saa 2:15 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Kocha huyo alitua nchini Jumanne iliyopita akitokea nyumbani kwao Tunisia akiwa na benchi lake jipya la ufundi akiwemo msaidizi wake, Sghir Hammadi kabla ya juzi kocha wa viungo, Jawad Sabri kutua akitokea Raja Casablanca ya Morocco.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, kocha huyo alianza kazi ya kukinoa kikosi hicho juzi Alhamisi saa kumi kamili akitumia saa moja sawa na dakika 60.Mtoa taarifa huyo kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, alisema kocha huyo alitumia saa Songne na Ditram Nchimbi.
Hivyo kwa sasa kwenye safu hiyo kazi ipo kwa washambuliaji hao kuwania nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza.
“Kocha ameanza kuifundisha timu jana (juzi) Ahamisi saa kumi kamili jioni na alitumia saa moja pekee sawa na dakika 60 ikiwa siku yake ya kwanza tangu atue nchini na asaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
“Akianza kibarua chake alianza na program mbili pekee za kiufundi iliyowahusisha mabeki na washambuliaji katika kuwaongezea mbinu, ufundi na kuwarejeshea hali ya kujiamini wakiwa ndani na nje ya 18 ya goli la wapinzani.“
Katika safu ya ulinzi mabeki moja kwa kuanza na program za kimbinu pekee katika kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Azam.
Alisema kuwa katika program hizo alianza na safu ya ulinzi iliyoongozwa na Mghana Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Kibwana Shomari na Adeyum Saleh kwa lengo la kutengeneza ukuta wa chuma utakaozuia na kupunguza mabao.
Aliongeza kuwa program nyingine aliyoifanya ni ya ushambuliaji kwa kuwaongezea mbinu za kiufundi jinsi ya kufunga na kutengeneza mabao iliyowahusisha washambuliaji wote, Mrundi Said Ntibazonkiza ‘Saido’, Michael Sarpong, Yacouba wenyewe walipewa mbinu ya jinsi ya kuwazuia wapinzani kupenya kwenye ngome yao kwa kuwazuia kuanzia umbali wa mita 21 ili wasilifikie goli lao huku akiwapa mbinu ya jinsi ya kuokoa mipira ya vichwa itakayotokana na krosi, faulo na kona,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassani Bumbuli kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Ni kweli kocha ameanza kibarua cha kuifundisha timu baada ya kusaini mkataba na kikubwa tumefurahia kuona wachezaji wakimpokea vizuri, hivyo Wanayanga wanatakiwa kuungana na kumpa ushirikiano kocha wetu mpya.
WILBERT MOLANDI,Dar es Salaam