×

Rais Magufuli Awatunuku Wahitimu JWTZ

magufuli-1

DAR ES SALAAM: Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli amewatunuku Cheo cha Luteni Usu wahitimu 194 wa mafunzo ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), hafla inayofanyika katika Viwanja vya Ikulu Jijini dar es Salaam.

magufuli-3

Wahitimu hao kati yao 168 ni wanaume na 26 ni wanawake, kwa ilivyozoeleka miaka ya nyuma walitakiwa kutunukiwa Cheo hicho katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi Monduli na badala yake hafla ya kuwatunuku imefanyika kwenye viwanja hivyo vya Ikulu, Dar.

magufuli-5

Mbali na Rais Magufuli, wageni wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Davis Mwamnyange, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John William Kijazi.

magufuli-7Kati ha wahitimu hao, 193 wamehitimu mafunzo hayo katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi Monduli huku mmoja akihitimu masomo hayo nchini Uingereza ambapo kwa mujibu wa taratibu za JWTZ hata kama amesoma nje ya nchi ni lazima aungane na wenzake atunukiwe akiwa hapa hapa nchini Tanzania na ndivyo ilivyofanyika.

Baada ya kutunukiwa vyeo hivyo wahitimu waliapa kiapo cha utii na kuvalishana nyota kwenye mabega yao huku kila mmoja akimvalisha mwenzake.

Baadaye sherehe zimeendelea viwanjani hapo huku, bras band ya jeshi imetumbuiza na kusherehesha kwa ngoma na matarumbeta yao.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

halotel-strip-1-1

 RAIS MAGUFULI KAMPIGIA SIMU MAKONDA KWENYE MKUTANO JUU YA BARABARA