×

Upinzani Washinda Urais Gambia

_92803539_81a3c62e-c6e2-4971-8132-5dd7a6feb203

Mgombea wa upinzani, Adama Barrow aliyeshinda urais kwa kupata kura 263,515.

Mgombea wa upinzani, Adama Barrow ameshinda uchaguzi wa urais nchini Gambia baada ya kupata kura 263,515 huku Rais Yahya Jammeh akipata kura 212,099.

Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini humo amemtangaza mgombea huyo wa upinzani kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.

_92804404_ap_jammeh

Rais Yahya Jammeh aliyepata kura 212,099.

Mwandishi mmoja wa habari kutoka shirika la Reuters anasema kuwa amezungumza na Adama Barrow ambaye amemuambia kuwa anasubiri simu ya kukubali kushindwa kutoka kwa Rais Jammeh.

_92804408_reuters

Mkuu wa tume ya uchaguzi akiongea na wanahabari amewaeleza kuwa Rais Yahya Jammeh ambaye ameitawala nchi hiyo kwa miaka 22 baada ya kuingia madarakani kwa njia ya mapinduzi atakubali matokeo hayo.

halotel-strip-1-1