×

Wagonjwa 14 wa Corona Waongezeka TZ, Wafikia 46

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema watu wengine 14 wamethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona nchini Tanzania na kufanya jumla ya kesi za maambukizi hayo zilizoripotiowa tangu ugonjwa huo uingie nchini kufikia watu 46.

 

Hayo yamebainishwa leo Jumatatu, Aprili 13, 2020 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, kupitia ripoti ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (Covid-19) nchini na kueleza kuwa wagonjwa 13 wametokea Dar es Salaam na mmoja ametokea mkoani Arusha.

 

Mchanganuo wa maeneo walipo waathirika wa virusi vya corona nchini #Tanzania;
Dar es Salaam: 32
Zanzibar: 9
Arusha: 3
Kagera: 1
Mwanza: 1
#StopCorona
#COVIDー19.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema wagonjwa saba wamepona ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na Corona Virus, huku idadi ya walioambukizwa ikiongezeka na kufikia 46 kutoka 32.

Leave a Comment