Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (kulia) akisalimiana na Rapa Shariff Thabeet maarufu kwa jina la Darassa alipotembelea leo ofisi za Global Publshers Bamaga Mwenge, Dar na kufanya mahojiano na Global TV Online.
Darassa (katikati) akiwa na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo (kushoto) na Eric Shigongo.
Mtangazaji wa Global TV Online, Kelvin Shayo (kushoto) akifanya mahojiano na Darassa.
… Akiendelea na mahojiano na Global TV.

Darassa akiwa katika pozi na wafanyakazi wa Global Publishers.
Darassa akiendelea na mahojiano na Global TV Online.
Sweetbert Lukonge
RAPA wa Muziki wa HipHop hapa nchini ambaye kwa sasa anabamba Ngoma ya Muziki, Shariff Thabeet maarufu kwa jina Darassa amefunguka kuwa anavutiwa zaidi na uchezaji wa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva ambao amekuwa akiuonyesha uwanjani.
Darassa aliyasema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na Global TV katika mahojiano maalumu yaliyofanyika katika studio za TV hiyo zilizopo Bamaga jijini Dar es Salaam.
Alisema mbali na kuvutiwa na uwezo wa kutandaza soka wa Msuva pia amewahi kucheza naye wakati walipokuwa wadogo katika Uwanja wa Kijitonyama Muslim jijini Dar es Salaam.
“Mbali na muziki pia napenda sana soka kwani kati ya michezo ambayo huwa inaniburudisha lakini pia jambo la kushangaza mimi nazipenda timu zote mbili ambazo zinamashabiki wengi hapa nchini, Simba na Yanga na huwa napata shida sana pindi zinapokutana uwanjani.
“Lakini katika timu hizo kunawachezaji ambao huwa napenda jinsi wanavyo cheza na mmoja kati yao ni Simon Msuva, huyu nimecheza naye tulipokuwa mdogo hakika yupo vizuri,” alisema Darassa na kuongeza kuwa:
“Mbali na Msuva pia nimecheza na Siad Ndemla aliyopo Simba kwa sasa pamoja Abdallah Seseme ambao pia nilikuwa nikisumbuana nao sawa tulipokuwa tukikutana uwanjani,” alisema Darassa.
MZEE WA MIAKA 76 ALEYETANAGAZA KUTAFUTA MKE “FULL EXLUSIVE INTERVIEW”