BURUNDI: Wanasiasa wa upinzani nchini Burundi walio uhamishoni wamepinga jitihada za aliyekuwa rais wa Tanzania Benjamin William Mkapa za kutatua mzozo uliomo nchini humo.
Hii imetokea baada ya William Mkapa kuwaambia waandishi wa habari nchini humo kuwa si jambo zuri kuendelea kutilia shaka uhalali wa Raia Pierre Nkurunzia.
Nchi ya Buurndi ilitumbukia kwenye mzozo baada ya bwana Nkurunziza kutangaza kuwa angewania muhula wa tatu.
Mamia ya watu wameuawa na maelfu kukimbia nchi kulipozuka ghasia.
Rais Mkapa alipewa jukumu la kusaidia kutatua mzozo huo, na amesema kuwa makubaliano yataafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.
Baadhi ya wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni wanatafutwa na serikali kwa kupanga maandamano ya kupinga hatua ya Rais Nkurunziza hatua ambazo serikali inazitaja kuwa za kihalifu. Wengine waliilaumiwa wa kushiriki kwenye mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli mwezi Mei.
CHANZO: BBC

