DAR ES SALAAM: Leo Desemba 9 Tanzania Bara imeazimisha miaka 55 tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa wakoloni mwaka 1961.
Maadhimisho hayo yamepambwa na shughuli mbalimbali za kijeshi lakini pia ngoma za asili kutoka kwa makundi mbalimbali pamoja na Rais Magufuli ambaye pia ni Amri Jeshi Mkuu kukagua Gwaride la uhuru, sherehe ambazo kitaifa zimeashimishwa kwenye Uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam.
Mbali na mambo hayo yaliyoonekana kuwavutia wengi, jambo lingine lililowafurahisha ni pale Rais Dk Magufuli alipoamua kutembea kiukakamavu kama mwanajeshi mara baada ya kumaliza kukagua gwaride katika maadhimisho haya ya 55 ya uhuru.
MZEE WA MIAKA 76 ALEYETANAGAZA KUTAFUTA MKE “FULL EXLUSIVE INTERVIEW”











