×

Gari la Mbongo Lamvuta Waziri Mpango

viwanda-1Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akiitazama gari iliyobuniwa na Mtanzania, Jacob Luis.

viwanda-2Mtanzania aliyetengeneza gari hilo, Jacob Luis, mkazi wa Vingunguti jijini Dar akimweleza jambo waziri Mpango.

viwanda-3Mpango na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Edwin Rutageruka wakiendelea kuliangalia gari hilo.

viwanda-4…Jacob Luis akiwa karibu na gari alilolibuni.

viwanda-5 Mmoja wa wananchi aliyefika kwenye maonyesho hayo akiliangalia gari hilo.

viwanda-6Mlemavu wa macho aitwaye Dk. Abdallah Nyangalio (kushoto) akiwaonyesha viongozi hao baadhi ya vitambaa anavyovitumia kushona nguo.

viwanda-7. ..Mpango akiangalia gauni lililoshonwa na Dk. Nyangalio.

viwanda-8 …Akimpatia mkono wa pongezi.

viwanda-9…Akiendelea kuangalia bidhaa zingine zilizokuwa kwenye maonyehso hayo.

viwanda-10Mtaalam wa masuala ya injini za magari, Mandela Makari naye akiwaelezea jambo wananchi waliofika kwenye banda lake.

Na Denis Mtima/GPL

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango jana ametembelea maonyesho ya viwanda, kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Sabasaba jijini Dar ambapo pamoja na mambo mengine alivutiwa na gari lililotengenezwa na Mtanzania, Jacob Luis.
Kamera yetu ilifika kwenye viwanja hivyo na kujionea maonesho ya bidhaa mbalimbali na ilipokuwa kwenye Banda la Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO), ilimshuhudia Dk. Mpango akiguswa na gari hilo kisha kumpongeza.

“Kwa kweli nikupongeze sana kwa ubunifu huu. Nimefurahi sana na kuhusu changamoto za kuliwezesha kuingia kwenye soko, kama serikali itakusaidia,” alisema Dk. Mpango.

Kama hiyo haitoshi, Dk. Mpango akiwa kwenye Banda la walemavu wasiona, kwanza alimpongeza mwalimu na mtaalamu wa kushona nguo na kuwafundisha walemavu wengine wa macho aitwaye Dk. Abdallah Nyangalio na kuahidi kuwasaidia fedha za kununua cherehani mbili kutoka katika mshahara wake ili kuwawezesha katika kujikwamua kiuchumi.

“Kuliko kuendelea kuwa ombaomba mtaani ni bora nyie mnaojiwezesha kwa kufanya kazi, hivyo serikali itaendelea kuwatia moyo na hamasa ili kuona ni jinsi gani walemavu mnaweza kuondokana na dhana iliyozoeleka ya kuwa nyie ni ombaomba pia naomba viwanda vinavyozalisha nguo viweze kuwasaidia japo vitambaa ambavyo hawavitumii, wawape kwa ajili ya walemavu wanaojifunza kuvitumia,” alisema Mpango.