Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia page yake ya Twitter jioni ya leo kimekanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Sekretarieti kuwa siyo sahihi na Kamati Kuu ya chama hicho haijafanya uteuzi wa mjumbe yeyote.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu iliyokutana leo tarehe 11/12/2016 Dar es salaam imejadili taarifa ya tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

