KLABU ya Simba ikiwa na kipa wake mpya Daniel Agyei, jana imekubali kichapo cha mabao 2-1 katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Simba ilikuwa na nafasi ya kusawazisha katika mechi hiyo lakini beki, Janvier Bokungu akakosa penalti. Kipigo cha Simba, kinapunguza makali ya watani wake Yanga ambao walichapwa kwa mabao 2-0 na JKU ya Zanzibar wikiendi iliyopita.


