×

Tundu Lissu Akamatwa tena na Jeshi la Polisi

lissuDAR ES SALAAM: Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu, Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa madai ya uchochezi.

“Nashikiliwa na polisi hapa Kituo Kikuu kutokana na ile press conference (mkutano na waandishi wa habari) kuhusu kupotea kwa Ben Saanane,” Lissu alimweleza mwandishi mmoja wa habari mapema leo kupitia simu.

Hivi karibuni, Lissu alifanya mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni jijini hapa, ambapo mbali na mambo mengine, alilitaka jeshi la polisi kuhakikisha linafanya kila liwezekanalo, kumtafuta kada maarufu wa chama hicho anayedaiwa kupotea, Ben Saanane.
Saanane ambaye ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe alipotea ghafla takribani mwezi mmoja sasa na hajulikani alipo.

Shigongo afundisha jinsi ya kupiga hela ndani ya serikali ya Magufuli