×

Achana na Akina Ronaldo na Messi, Huyu Ndiye Mwabnasoka Atakayalipwa Pesa Nyingi Zaidi Duniani

chelsea-v-stoke-oscar-celeb_3073049

Oscar atakuwa ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi duniani akifanikiwa kuhamia Ligi Kuu ya China ambako mpaka sasa bado vitu vichache ili aweze kujiunga huko.

Oscar mwenye umri wa miaka 25, anayekipiga kwenye Klabu ya Chelsea ya Nchini Uingereza, anatarajia kuhama mwezi mwezi ujao (Januari 2017) na kuelekea kunako Klabu ya Shanghai SIPG kwa mkataba unaogharimu Euro Mil. 52.

Kwa usajili huo, raia huo, mwanasoka huyo ambaye pia ni tegemeo la Timu ya Taifa ya Brazil ataweka rekodi ya mchezaji atakayekuwa akilipwa pesa nyingi zaidi duniani ambapo atakuwa akilipwa kitita cha Euro 400,000 (sawa na Tsh. Bilioni 1.1) kwa wiki, maana yake ni kwamba, Euro milioni 20.8 kwa mwaka ambazo ni sawa na ( £57,143 kwa siku. Au £2,381 kwa saa. Au £39 kwa dakika).

Aidha Meneja wa Chelsea, Antonio Conte asema Ligi Kuu ya China ni hatari kwa timu zote, kutokana na kiasi kikubwa cha fedha wanacholipa wachezaji na pengine itakuja kuwa Ligi yenye ushindani mkubwa kwa miaka ijayo.

Wachezaji 10 wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani

1) Oscar (Shanghai SIPG) £400,000 kwa wiki £20.8 milioni kwa mwaka*

2=) Cristiano Ronaldo (Real Madrid) £365,000 kwa wiki£19 milioni kwa mwaka**

2= Lionel Messi (Barcelona) £365,000kwa wiki £19 milioni kwa mwaka**

4) Gareth Bale (Real Madrid) £346,000kwa wiki £18 milioni kwa mwaka**

5) Hulk (Shanghai SIPG) £317,000kwa wiki £16.5 milioni kwa mwaka

6) Paul Pogba (Manchester United) £290,000kwa wiki £15 milioni kwa mwaka

7) Neymar (Barcelona) £289,000kwa wiki £15 milioni kwa mwaka**

8=) Graziano Pelle (Shandong Luneng) £260,000 pkwa wiki£13.5 milioni kwa mwaka

8=) Wayne Rooney (Manchester United) £260,000kwa wiki £13.5 milioni kwa mwaka

10) Zlatan Ibrahimovic (Manchester United) £250,000kwa wiki £13 milioni kwa mwaka.

great-hull-chinaWachezaji  wengine maarufu wanaokipiga Ligi Kuu ya China

GERVINHO (HEBEI CHINA FORTUNE): Aliwahi kuzichezea Arsenal na Roma.

STEPHANE M’BIA ( HEBEI CHINA FORTUNE): Aliwahi kuzichezea  QPR, alikuwa Kapteni wa Cameroon kwenye Kombe la Dunia ameshinda Europa League mara mbili akiwa na Sevilla.

OBAFEMI MARTINS (SHANGHAI SHENHUA): Aliwahi kuichezea Birmingham City.

DEMBA BA (SHANGHAI SHENHUA): Amepita West Ham, Newcastle United na Chelsea, Mseenegal mwenye miaka 31, straiker aliyecheza kwenye nchi sita tofauti.

GAEL KAKUTA (HEVEI CHINA FORTUNE):Aliichezea Chelsea akahamia China akiwa na miaka 25.

GRAZIANO PELLE (SHANDONG LUNENG): Alitokea Southampton kwa uhamisho ulitengeneza faida ya Euro milioni £5.

 EZEQUIEL LAVEZZI (HEBEI CHINA FORTUNE): Alitokea Paris Saint-Germain mnamo Februari. Ni Muargentina anayelipwa zaidi ya £300,000 kwa wiki.

HULK (SHANGHAI SIPG): Alitokea Zenit.

RAMIRES (JIANGSU SUNING): Mkataba wa £25 milioni ulimtoa kunako klabu ya  Chelsea mnamo Januari anakumbukwa kwa bao lake aliloifunga Barcelona mwaka 2012

ALEX TEIXEIRA (JIANGSU SUNING): Ana miaka 26 ametokea klabu ya Shakhtar Donetsk.

JACKSON MARTINEZ (GUANGZHOU EVERGRANDE): Amezichezea Porto na Atletico Madrid.