×

Madai, Dude Ahamia Rasmi kwa Ester Kiama

      ofm-wamnasa-dude-kwa-ester-kiama-8Stori inatoka Gazeti la AMANI

DAR ES SALAAM: Kweli OFM Kiboko! Kumekuwepo na madai kwamba, mwigizaji nyota wa sinema za Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ sasa anaishi rasmi Kijitonyama kwa msanii mwenzake, Ester Kiama na mapenzi motomoto yameshamiri, Amani limenyetishiwa.

ester-kiama-3Ester Kiama

Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, Dude anaishi nyumbani kwa mwigizaji huyo huku akiendelea kumdanganya mkewe kwamba, anakuwa kwenye kushuti filamu.

“Ukweli ninaotaka kuwaambia mimi ni huo. Dude anaishi kwa Ester. Inaonekana akitoka nyumbani kwake, Jet Lumo anamuaga mkewe, Eva kwamba anakwenda kushuti sinema. Sasa si unajua, sinema inaweza kushutiwa hata siku kumi.

“Kwa hiyo ina maana siku ya saba akirudi nyumbani, Eva anajua jamaa anatoka ‘lokesheni’, kumbe kwa mke mwenzake. Halafu yule Eva ni mtu wa ajabu sana, yaani katika hali kama hii, kila akiambiwa na mashoga zake, anakataa akisema Dude na Ester wanakutana kwa sababu ya sanaa tu.      Hajui, ndiyo maana wenzake wanamng’ong’a,” kilisema chanzo.

ofm-wamnasa-dude-kwa-ester-kiama-2Kamanda wa Kikosi cha OFM akiongea na Ester Kiama nje ya nyumba yake.

Kikaongeza: “Unajua nini? Mwanamke kama Eva yeye anakuwa hajui kama anaibiwa. Hasa kama mume atakuwa haoneshi mabadiliko ndani mpaka kitandani. Ester yeye anajua kwamba anaiba. Kwa hiyo asipomwona Dude siku mbili anajua yuko kwake, hana neno. Eva yeye asipomwona anajua yuko lokesheni.”

Ili kupata uhakika wa madai haya kwamba, Dude anaishi kwa Ester na kwake pia, kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kilipewa jukumu la kumfuatilia Dude ili kubaini ukweli au uongo wa madai hayo.

Jumatatu iliyopita, OFM wasiojulikana na Dude walifika nyumbani kwa Ester na kugonga geti kubwa ambapo Ester ndiye aliyetoka kufungua.

Ikawa hivi…

OFM: Samahani, sisi ni wasanii tunatokea Geita. Tunamtafuta Dude kwa ajili ya kufanya naye filamu, sasa kuna mtu kasema anaishi hapa.”

ofm-wamnasa-dude-kwa-ester-kiama-1OFM akiwa getini kwa Ester.

Ester: “Kwanza nani kawaelekeza hapa?”

OFM: “Unajua tumemtafuta Dude karibu mwezi mmoja sasa. Kuna rafiki yangu msanii, ndiyo akatuelekeza kwamba anaishi hapa kwako.”

Ester: “Ooo! Ni kweli, anaishi hapa. Sasa hivi hayupo, ngoja nimpigie simu, nadhani hayupo mbali. Mimi natoka.”

OFM: “Tutashukuru sana dada.”

Ester: “Msijali.”

Ester alichukua simu yake akampigia Dude…

“Uko wapi? Kuna wasanii wanakutafuta hapa…mimi natoka kwa hiyo siwezi kukaa nao.”

Baada ya kumpigia simu Dude, Ester aliwaambia OFM wasubiri, yeye akatoka na gari aina ya Toyota Mark X lenye namba T 244 CVL kisha akasimama nje ya geti na kuwapa OFM namba za simu za Dude licha ya kwamba, OFM wanazo.

ofm-wamnasa-dude-kwa-ester-kiama-3Dude akiingia ndani kwa Ester

Dakika tatu mbele baada ya Ester kuondoka, Dude akatokea akiwa kwenye gari aina ya Toyota Mark II lenye namba za usajili T 452 BNG.

Alishuka kwenye gari kisha akabadili nguo ya juu. Alivua shati jeupe na kuvaa fulana nyeusi yenye maandishi ya kijani yaliyoandikwa Kura Yangu Kwa Magufuli, chini akiwa na pensi ya jinsi.

ofm-wamnasa-dude-kwa-ester-kiama-4…Akizungumza na OFM

Yeye na OFM wakakaa kwenye pub moja jirani na nyumba hiyo. Mazungumzo yakawa hivi baada ya salamu:

OFM: Sisi ni wasanii, tumetokea Geita. Tunataka kukushirikisha kwenye filamu yetu. Tumekutafuta tukaambiwa unaishi hapa.”

Dude: “Ni kweli, niko hapa. Sasa mimi niko tayari. Ni maelewano tu.”

OFM: “Sijui utatufanyia shilingi ngapi? Maana tunataka ucheze kama steringi.”

ofm-wamnasa-dude-kwa-ester-kiama-5Dude: “Mimi nipeni milioni tatu tu nitacheza mwanzo mwisho.”

OFM wakajifanya wanalialia pale wakimuomba Dude apunguze mpaka laki saba (700,000), naye akakomaa mpaka baadaye akasema atakubali kwa milioni moja na nusu (1,500,000).

OFM: “Basi sasa tunakwenda lakini kesho asubuhi (Jumanne) tutakupigia simu baada ya kuongea na bosi wetu.”

Dude: “Sawa.”

ofm-wamnasa-dude-kwa-ester-kiama-6Lakini kabla hawajaondoka, OFM mmoja alimuomba Dude maji ya kunywa ili kuona kama ataweza kwenda nyumbani kwa Ester bila shaka. Ikawa hivyo, alisimama, akaongozana na OFM huyo, wakaingia ndani huku Dude akimkaribisha sana na mazungumzo ya hapa na pale. Alichukua maji kwenye friji na kumpa OFM, akanywa na kuondoka akiwa amemwachia Dude namba za simu.

ofm-wamnasa-dude-kwa-ester-kiama-7Kesho yake, Jumanne asubuhi, Dude alimpigia simu OFM na kumuuliza kama alizungumza na bosi wake kuhusu dili  waliloongea.

OFM: “Kaka hakuna cha dili wala nini, sisi ni OFM na tulikuwa tunakuchunguza kama ni kweli unaishi pia kwa Ester.”

Dude: Daah! (anaonesha mshtuko)… kwa hiyo umefanikiwa ulichokuwa unakichunguza?

OFM: Ndiyo.

Dude: Basi nashukuru sana kaka, ila daah!

Ili kuweka sawa mzani wa madai, OFM ikaanza na Eva, ambapo ilimpigia simu kuzungumza naye kuhusu Dude kuishi kwake na kwa Ester.

“Mimi ninachojua wanacheza wote filamu tu. Lakini kwamba anaishi kwa Ester sijui. Hata sasa hivi alikuwepo hapa, ametoka, nadhani amekwenda kazini.

“Ila watu wengi wamekuwa wakiniambia habari za huyo dada. Kwani anataka umaarufu au? Maana kama ni umaarufu hawezi kuupatia kwa Dude. Nilishakaa na Dude akaniambia hakuna kinachoendelea kwenye mapenzi,” alisema Eva.

Baada ya Eva, OFM likampigia simu Ester. Simu ya Ester iliita wee, baadaye akapokea ambapo aliposomewa mashtaka hayo, aliwaka:

“Nyie hamna maswali mengine ya kuniuliza zaidi ya Dude, kila siku mnauliza jambo hilohilo tu! Tafuteni maswali mengine, siishi na Dude, anaishi kwake na mimi naishi kwangu, tunakutanishwa na kazi tu.”

 Dude na Ester wamekuwa kwenye midomo ya wadau wakisadikiwa kuwa ni wapenzi na kwamba, ishu ya kucheza filamu ni kisingizio tu. Waandishi wetu waliwahi kumzukia Dude kwa Ester miezi ya nyuma lakini akajitetea kwamba ni filamu tu.

Kuna wakati Dude alimkutanisha mkewe, Eva na Ester kwa lengo la kukata mzizi wa fitina na kusema hawezi kutoka na mrembo huyo wakati ana mke.

Kwa safari hii, haiingii akilini Dude aseme ni filamu kiasi cha kuweza kuigia nyumbani kwa mwanadada huyo mwenyewe akiwa hayupo na kumpa mgeni maji. Lakini pia katika mazungumzo, OFM walimwambia Dude kwamba wamesikia anaishi pale, akakubali, Ester naye alikiri.

NILIPIGWA NA MGAMBO NIKAPOTEZA MTAJI WANGU, MAKONDA NISAIDIE MAISHA MAGUMU