×

Nisha Adaiwa Kuua Kichanga

nishaaStori: Mwandishi Wetu | Gazeti la Ijumaa, Toleo la Desemba 23, 2016

MSANII wa fi lamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ anadaiwa kuua kichanga kilichokuwa tumboni baada ya hivi karibuni kujitangaza ana mimba kubwa ya miezi mitano kisha baadaye akaibuka na kudai kuwa, eti hakuwa na mimba.

ISHU ILIPOANZIA

Novemba 15, mwaka huu zilivuja taarifa kuwa, msanii huyo ana mimba kubwa tu na ameamua kukimbilia nchini China kutokana na utata wa mhusika wa ‘mzigo’ huo.

Baada ya habari hizo kuzagaa mitandaoni ikiwa ni pamoja na Nisha mwenyewe kutupia picha ikimuonesha ana mimba kwenye ukurasa wake wa Instagram, mwandishi wetu alifanya

jitihada za kumpata ili kuweka wazi kuhusu ujauzito huo.

Alipopatikana kupitia namba yake ya WhatsApp, Nisha akijua kabisa anaongea na mwandishi wa habari, alimthibitishia kuwa ana mimba ya miezi mitano lakini ameipata kwenye mazingira tata ndiyo maana aliamua kufanya siri.

“Ni kweli nina ujauzito, kuna mambo yako nyuma ya pazia ya mimba hii ila nikirudi Bongo kila kitu kitakuwa wazi,” alisema Nisha.

nishaSalma Jabu ‘Nisha’

ADAIWA KUTAKA KUITOA

Ilidaiwa na mtu wa karibu na msanii huyo kuwa, kutokana na mwanaume aliyempa mimba hiyo kutokuwa na ‘future’ naye na kwa kuwa aliipata bila kutarajia, alikuwa akifi kiria kuitoa ila hofu yake ikawa kwenye kuhatarisha maisha yake.

VYOMBO VYA HABARI VYALA NAYE SAHANI MOJA

Mara baada ya kutangaza mwenyewe kuwa ana ujauzito mkubwa, ‘media’ mbalimbali zilianza kumuandika huku mwenyewe akitoa ushirikiano.

AIBUKA, ADAI HAKUWA NA MIMBA

Cha kustaajabisha hivi karibuni mdada huyo bila aibu aliibukia kwenye chombo kimoja cha habari na kueleza kuwa, eti hakuwa na mimba bali alijitangaza hivyo kwa sababu alizozijua mwenyewe.

Maelezo yake hayo yaliibua hasira kutoka kwa wadau mbalimbali wakihoji sababu za kuwadanganya ambapo baadhi walikwenda mbele zaidi na kusema kuwa, kuna uwezekano mkubwa alikuwa nayo na akafanikiwa kuitoa.

“Huyu lazima atakuwa ameua kichanga kilichokuwa tumboni, anatakiwa kufuatiliwa kwani imekuwa ni mchezo sasa kwa mastaa kutoa mimba hata zile kubwa,” alisema Mama Sasha wa Sinza jijini Dar.

Naye Salum K ambaye hakujitambulisha anatokea wapi alipoiona habari mtandaoni ya kwamba eti Nisha hakuwa na mimba, alikomenti hivi; “Huu ni ulimbukeni, afuatiliwe maana kama alikuwa anajua anaongea na chombo cha habari halafu akathibitisha

kuwa ana mimba akiambatanisha na picha, sasa leo akisema hakuwa na mimba?

NISHA ANASEMAJE?

Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Nisha na kumbana juu ya madai kuwa, alikuwa na mimba kubwa tu lakini ameitoa ambapo alisema: “Mimi sijatoa mimba, lile tumbo kwenye ile picha nililitunisha kisha nikajipiga picha.” Alipoulizwa sababu ya kuudanganya umma, alibaki kujiumauma tu.

Zaidi kuhusu habari hii nenda ukurasa wa 10.

Duh! Hii Kali, Sangoma Anaswa Akimroga Darassa!