×

Benki Kuu Yakanusha Taarifa Kuhusu Noti ya TZS 500 Kutotumika Tena Baada ya Disemba 31, 2016

tzsh-500Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa habari inayoenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano haitatumika tena baada ya Disemba 31, 2016 sio taarifa ya kweli na ni uvumi unaopaswa kupuuzwa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za kibenki BoT, Marcian Kobello ambapo alifafanua kuwa noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi.

Aidha, Kobello amewataka wananchi kupuuza taarifa zinazoeleza vinginevyo kwani si za kweli.

Serikali iliamua kuleta sarafu ya TZS 500 baada ya kuwepo malalamiko kuwa noti ya TZS 500 ambayo ndiyo inazunguka zaidi inachakaa mapema sana.

***********************

TAARIFA YA MKURUGENZI WA HUDUMA ZA KIBENKI BOT

Benki kuu ya Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa,habari inayoenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano  haitatumika tena kuanzia Desemba 31,2016; sio taarifa ya kweli na ni uvumi unaopaswa kupuuzwa.

Ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi. Tafadhali mpuuze taarifa hizo sio za ukweli.

Marcian Kobello. 

Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki- BoT .

ILIKUPITA HII?

Mpaka Home; Haya Ndo’ Maisha Halisi ya Darassa, Cheki Video Akipika Msosi Gheto