Leo ni siku ya Boxing day kimenuka nchini Ubelgiji katika Klabu ya KRC Genk anayecheza Mtanzania Mbwana Ally Samatta imeamua kuachana na kocha wake Peter Maes baada ya kumtimua kazi kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo ambayo timu imekuwa ikiyapata.
Habari kutoka kwenye tovuti maalum ya club ya KRC Genk imetoa taarifa kuhusu kumaliza ushirikiano na kocha huyu baada ya kuanza kuifundisha club hii tangu msimu wa 2015/2016.
Kocha huyu alianza majukumu ya kuifundisha club ya Genk mwaka 2015 hivyo basi ndiye kocha wa kwanza kumpokea Mbwana Samatta kwenye soka la Ulaya.
Genk wamemtakia maisha mema kwenye majukumu yake mengine na maisha baada ya Genk.
Genk wapo katika nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi kuu ya Ubelgiji wakiwa na alama 25 huku wakiwa wameruhusu magoli mengi na pia wamefuzu kucheza hatua ya mtoano ya 32 ya Europa League ambayo inatarajia kuchezwa Februari 15 au 16 mwakani na wataanza na timu ya Romania ugenini.