×

Nguli wa Muziki wa Pop Duniani, George Michael Afariki Dunia

george-michaelMWANAMUZIKI nguli mwenye asili ya Uingereza, ambaye alijizolea umaarufu mnamo miaka ya 1980 na kuwika ulimwenguni kutokana na mtindo muziki wake wa mahadhi ya Pop, amefariki dunia jana Desemba 25, 2016 akiwa na umri wa miaka 53, nyumbani kwake.

british-singer-george-michael-performs-o Msemaji wa mwanamuziki huyo amearifu kwamba nguli huyo aliaga dunia akiwa nyumbani kwake Oxfordshire akiwa amelala baada ya moyo kushindwa kufanya kazi, na kuongeza kuwa Michael hakuwa mgonjwa kabla ya mauti yake.

George Michael amesifika kwa kuuza nakala zaidi ya milioni 100 za albamu zake huku Kundi lake la muziki la Wham lilijipatia umaarufu ulimwengu mzima na kupata mafanikio makubwa kwa tungo zao kama ‘Wake Me Up Before You Go-Go’ na ‘Careless Whisper’

george-michael-leaving-his-home-in-north-london-britain-17-oct-2012Kundi hilo lilijizolea umaarufu na kuwa kundi la kwanza la Magharibi kwa miondoko ya Pop kufanya onesho la kimuziki nchini China.

Bendi hiyo iliposambaratika, George Michael aliendelea kujizoelea umaarufu akiwa mwanamuziki wa kujitegemea.

Katika kipindi cha muongo uliopita alikuwa akisumbuliwa na maradhi yasababishwayo na utumizi wa dawa za kulevya, ikiwemo kuendesha gari kwa kasi na kupoteza mwelekeo na kuingia kwenye duka mjini London huku akiwa amelewa dawa za kulevya.

Mpaka Home; Haya Ndo’ Maisha Halisi ya Darassa, Tazama Anavyopika Msosi Gheto