×

DIAMOND PLATNUMZ & WASAFI CLASSIC: Shoo Ya Vodacom Wasafi Festival Yaacha Historia Mkoani Iringa

Usiku wa Dec 25, 2016  wakali wa Bongo Fleva akiwemo Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen, Q Boy, Chege pamoja na msanii kutoka Nigeria Kcee wameandika historia katika mkoa wa Iringa.

Shoo hiyo iliyopewa jina la Vodacom Wasafi Festival imefanyika katika uwanja wa Samora Stadium, hizi ni baadhi ya picha kutoka mahali palipofanyika tamasha hilo.

Sikukuu ya Krismasi ilikuwa ya aina yake kwa wakazi wa Iringa ambapo timu nzima ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, ikiongozwa na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, iliweka historia ya aina yake kwa kusepa na vijiji ndani ya Uwanja wa Samora, Iringa Mjini.

Idadi kubwa ya watu waliofurika kwenye shoo hiyo, iliweka historia ya aina yake kwa sababu si kawaida kwa uwanja huo kujaa kama ilivyotokea Jumapili ambapo timu nzima ya Wasafi, ilikamua shoo ya nguvu kinomanoma.

Rayvan, Harmonize, Rich Mavoco, Queen Darlin na wasanii wengine kibao, walizikonga vilivyo nyoyo za wakazi wa Iringa, huku wengi wakisikika wakipaza sauti zao kuwataka WCB waandae shoo nyingine mjini humo.