Bodi ya Wakurugenzi wa Timu ya Azam wamesitisha mikabata na makocha wake na benchi zima la ufundi wa klabu hiyo likiongozwa na Kocha wake Mkuu, Zeben Hernandez kutoka nchini Hispania kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.Azam FC iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 17. Ambapo katika mechi 17 za Ligi Kuu Bara, Azam FC imechinda mechi saba, imepoteza nne na sare sita, hali ambayo wazi inaonekana kutoufurahisha uongozi wa Azam FC hata kidogo.
Mpaka sasa Azam inafikisha makocha 9 tangu ipande daraja kuingia ligi kuu misimu iliyopita ikiwa ni wastani wa kocha mmoja kila msimu.