
Nelly Mwangosi (kulia) akisalimiana na Sifael Paul kabla ya kuanza mahojiano na Global TV.

Nelly Mwangosi akiongea jambo.

Mtangazaji wa Global TV Online, Kelvin Shayo (kulia) akifanya mahojiano na mshindi huyo.

Mahojiano yakiendelea.

Nelly Mwangosi akiishukuru Global Publishers na kuwashauri wasomaji kushiriki kwa wingi awamu ya pili ya Shinda Nyumba.

Mume wa Nelly Mwangosi, Karolo Stephen Magani akiongea na Global TV.
PICHA: MUSA MATEJA/GPL
Unamkumbuka mshindi wa awamu ya kwanza ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba, Nelly Mwangosi? Leo ametembelewa na uongozi wa Kampuni ya Global Publishers kwenye nyumba aliyojishindia ambayo ndiyo anayoishi kwa sasa, iliyopo Salasala jijini Dar es Salaam.
Nelly ambaye kabla ya kushinda nyumba hiyo alikuwa akiishi mkoani Iringa, kwa mara nyingine ameishukuru Global Publishers kwa kuyabadilisha maisha yake na kuwashauri wasomaji wengine, kushiriki kwa wingi ili nao maisha yao yabadilike kama ilivyotokea kwake.
Nelly amewashauri Watanzania wote kwa jumla, bila kujali itikadi zao au mikoa wanayotokea, kuichangamkia fursa hiyo kwa sababu hata yeye alipoisikia kwa mara ya kwanza, alikuwa haamini kama kweli anaweza kushinda lakini alipoanza kushiriki, aliendelea mpaka hatua ya mwisho na kilichotokea ni kwamba maisha yake yamebadilika kabisa.
“Najua kwenye ile awamu ya kwanza wapo watu wengi ambao walikuwa wakishiriki kama nilivyokuwa nafanya mimi, sasa mimi nawashauri kuitumia fursa hii ya pili kikamilifu kwa sababu huwezi kujua nani ataibuka mshindi. Mimi sikuwahi kudhani kama nitaibuka mshindi lakini ndiyo hivyo tena, nikashinda.
“Nawashauri watu kutoka kila kona ya nchi washiriki, huwezi kujua itakuwa zamu ya nani. Kama mimi niliweza kushinda nikiwa Iringa, kwa nini msomaji mwingine ashindwe kupata bahati kama mimi? Jamani nawaombamshiriki, huwezi kujua Mungu amekuandikia nini,” alisema Nelly kwa furaha.
Mbali na mambo mengine, uongozi wa Global Publishers pia ulimkabidhi Nelly zawadi ya runinga, ili kumfanya aendelee kuyafurahia maisha yake ndani ya nyumba mpya.
