The House of Favourite Newspapers

Mwangosi Alivyokabidhiwa Nyumba Yake Salasala, Dar

0

Mshindi wa Nyumba (2)

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo James (kushoto) akisoma mkataba wa makabidhiano ya nyumba aliyojishindia Nelly Mwangosi (wa pili kushoto).

Mshindi wa Nyumba (3)

Shigongo akizidi kuuelezea mkataba huo kabla ya kusainiwa.

Mshindi wa Nyumba (4)

Mshindi wa nyumba ya Global, Nelly Mwangosi akiweka saini katika mkataba wa makabidhiano ya nyumba hiyo.

Mshindi wa Nyumba (5)

Mume wa Nelly Mwangosi, Karolo Stephen Magani akiweka saini kama shahidi wa mshindi kwenye mkataba wa makabidhiano.

Mshindi wa Nyumba (6)

Karolo Stephen akimalizia kuweka saini.

Mshindi wa Nyumba (7)

Eric Shigongo naye akiweka saini kwa niaba ya Kampuni ya Global Publishers Ltd.

Mshindi wa Nyumba (8)

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho akiweka saini kama shahidi wa Global.

Mshindi wa Nyumba (10)

Shigongo akimkabidhi Nelly Mwangosi ufunguo wa nyumba yake.

Mshindi wa Nyumba (9)

Shigongo akimkabidhi Mwangosi mkataba wa makabidhiano ya nyumba hiyo.

Mshindi wa Nyumba (1)

….Akimpatia kadi kwa ajili ya malipo ya umeme.

MATUKIO MENGINE YA MSHINDI WA SHINDA NYUMBA

Nelly Mwangosi Akabidhiwa Nyumba Yake ==>http://bit.ly/2agFxmO

Mwangosi Atua Global, Kukabidhiwa Nyumba Leo =>http://bit.ly/2apkQ63

Nelly Mwagosi: Nahamia Dar ‘soon’ ==>http://bit.ly/2abOR8H

MWANAMAMA Nelly Mwangosi ambaye ndiye mshindi wa Shindano la Shinda Nyumba lililokuwa likiendeshwa na Kampuni ya Global Publishers kupitia magazeti yake ya Championi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Uwazi na Amani jana alikabidhiwa rasmi nyumba yake iliyopo Salasala jijini Dar es Salaam.

Mwangosi ambaye ni mkazi wa mkoani Iringa aliibuka mshindi wa nyumba hiyo katika bahati nasibu iliyofanyika Juni 30, mwaka huu katika Viwanja vya Mbagaga-Zakheem jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuiona nyumba hiyo ya kisasa, Mwangosi alishindwa kujizuia na kujikuta akibubujikwa na machozi ya furaha yaliyomfanya mume wake aanze kumbembeleza. Kitendo hicho pia kiliwatoa machozi baadhi ya ndugu zake aliokuwa ameambatana nao lakini baada ya kutulia alishuka katika gari aliyokuwa amepanda na kwenda moja kwa moja kukabidhiwa nyumba yake hiyo na Mkurugenzi wa Global, Eric Shigongo.

Baada ya zoezi hilo, Mwangosi aliishukuru Global Publishers kwa zawadi hiyo ambayo hakuwa anaitarajia katika maisha yake.

“Nawashukuru sana Global Publishers kwani mmeyabadilisha maisha yangu hakika Mungu awabariki wote, pia nachukua nafasi hii kuwataka Watanzania wote kutopuuzia bahati nasibu yoyote inayoendeshwa na kampuni hii.

“Hakuna uongo wowote unaofanywa ila kila kitu wanachokifanya ni kweli kabisa, katika maisha yangu sikuwa na ndoto za kumiliki nyumba lakini kupitia gazeti moja tu la Sh 500 maisha yangu yamebadilika, nawaomba Watanzania wote kushiriki bahati nasibu zote zinazoendeshwa na Global, ipo siku nao watafanikiwa,” alisema Mwangosi.

Katika hatua nyingine, Shigongo alimtaka Mwangosi kutokuwa na hofu kwani nyumba hiyo ni mali yake kuanzia leo na hakuna mtu yeyote atakayemsumbua.

“Nyumba hii kuanzia sasa ni mali yako, hivyo kuwa na amani kabisa hakuna atakayekusumbua, ila jambo la msingi unapaswa kumshukuru Mungu kwani amekufuta machozi kutokana na shida mbalimbali ulizopitia katika maisha yako.

“Siku zote nilikuwa namuomba Mungu mshindi wa nyumba hii awe ni mama ambaye maisha yake ni ya chini na asiye na nyumba kabisa na hatimaye maombi yangu yamesikika,” alisema Shigongo.

Bahati nasibu ya shindano hilo iliendeshwa kwa takriban miezi sita kwa kujumuisha wakazi wa mikoa yote ya Tanzania.

Shindano hilo pia lilijumuisha droo ndogondogo kwa kutoa zawadi kwa wasomaji ambapo baadhi yao walibahatika kujishindia pikipiki za kisasa, vyombo vya jikoni, mashuka, televisheni za ‘flats creen’, ving’amuzi vya Ting, simu za ‘smartphone’ na kadhalika.

MATUKIO MENGINE YA MSHINDI WA SHINDA NYUMBA

Nelly Mwangosi Akabidhiwa Nyumba Yake ==>http://bit.ly/2agFxmO

Mwangosi Atua Global, Kukabidhiwa Nyumba Leo =>http://bit.ly/2apkQ63

Nelly Mwagosi: Nahamia Dar ‘soon’ ==>http://bit.ly/2abOR8H

Leave A Reply