
Vibao vinavyoonyesha Barabara ya Azikiwe kufungwa kwa ajili ya ukarabati.

Eneo dogo la Barabara ya Azikiwe jijini Dar es Salaam imefungwa kwa muda kupisha ukarabati wa miundombinu ya barabara.

Ofisa wa Kampuni ya Group Six International Ltd inayokarabati barabara hiyo, Gilbert Lameck, akiwa kazini.
Mtandao huu ulizungumza na mmoja wa wasimamizi wa ujenzi huo ambaye ni Mtaalam wa Afya, Usalama, Mazingira na Viwango Mahali pa Kazi wa Kampuni ya Group Six International Ltd, Gilbert Lameck, ambaye alisema kuwa wamefunga kipande hicho kwa ajili ya ukarabati wa kupitisha bomba la maji taka na maji safi yanayotuama nyakati za mvua eneo la stendi ya daladala ya Posta Mpya akisema ujenzi huo utakamilika ndani ya muda mfupi.
“Ni ukarabati wa kawaida tu ambao tunaufanya kwa ajili ya kufanya mazingira yawe rafiki pindi mvua zinaponyesha na mabomba haya yaweze kutumika kusafirisha maji,” alisema Lameck.
NA DENIS MTIMA/GPL