×

Wanaodaiwa kumuua Mashali, bado hali tete

mashali-4 mashali-6 mashali-8 mashali-9 mashali-11 mashali-13

Watuhumiwa wanaodaiwa kumuua aliyekuwa bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali wakitoka mahabusu na kwenda kusikiliza kesi yao.mashali-25 mashali-26

…Wakitoka kwenye chemba ambako kesi yao ilikuwa ikisikilizwa.mashali-28 mashali-34

…Wakirudishwa lupango

DAR ES SALAAM: BADO ile kesi inayowakabili watuhumiwa saba wanaodaiwa kumuua aliyekuwa bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali, imezidi kupigwa kalenda baada ya watuhumiwa hao jana Jumanne kupandishwa tena kizimbani kwa mara ya tatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni iliyopo Kinondoni jijini Dar.

Watuhumiwa hao ambao ni Issa Kasim Swadaka, Ramadhani Ally, Athuman Bakari, Charles Fadhili Manongi, Mohammed Kassim Kyamba, Joseph Yacob Maro na Emmanuel Michael Paschal, awali walipandishwa kizimbani Desemba 8, mwaka jana, kisha wakapandishwa tena Desemba 20.

Kesi  hiyo namba IP 29 inayosimamiwa na Hakimu, Boniface Lyamwike huku mwendesha mashitaka akiwa ni Monica Ndakidema, imeahirishwa mpaka Januari 17, mwaka huu, huku upelelezi ukiendelea kufanyika.

Ikumbukwe kuwa, Oktoba 30, mwaka jana, Mashali aliaga dunia baada ya kupigwa na watu wasiojulikana huko Kimara jijini Dar es Salaam na mwili wake kuzikwa Novemba 2, katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.