×

Singeli/ “Mdogo Mdogo” ya Diamond Inahusiana na ‘Mashetani’

singeli03 MWAKA 2016 umemalizika katika hali ya mapinduzi makubwa katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya. Muziki wa Singeli kama sehemu mpya ya muziki wa kizazi kipya ambao unamepata mashiko sana maeneo ya Uswahilini jijini Dar es Salaam na sehemu zingine ya nchi yetu, muziki huu unabainika kuwa na mizuka ya ajabu inayohamisha fahamu za waimbaji na wachezaji wa muziki wa aina hii. Ni muziki unaomshawishi mchezaji na mwimbaji kucheza kwa kumwaga radhi ama kwa kujitupatupa na kutapatapa huku na huko.

singeli-1Pungwe ni ngoma ya asili inayochezwa na makabila ya ukanda wa kati, mikoa kama Dar es Salaam, Pwani na baadhi ya maeneo ya Morogoro. Upande wa visiwani Zanzibar, Pungwe ni ngoma inayopendwa zaidi na wazawa wa huko visiwani. Ngoma hii inayochezwa kwa namna ya kipekee, huanza kwa kutikisa kichwa pekee kwa hali ya kupandisha mizuka ya kishetani kwa watoto wa kike kwa kucheza bila ufahamu na baada ya ngoma kuisha mtu fahamu humrejea kisha anakuwa hajui ni nini alikuwa akifanya.

singeliNgoma hii huchezwa wakati wa harusi na baadhi ya makabila huicheza kwa shughuli maalum kama vile miviga na shughuli za kiganga.

Muziki wa Singeli umebainika kuwa na mfanano wa moja kwa moja na ngoma hii ya Pungwe, japo muziki huu huchezwa si kwa sherehe maalum za kijadi bali muziki huu ni kama muziki wa kizazi kipya na waimbaji wake huwa kama waimbaji wa muziki wa kizazi kipya.

Singeli kwa sasa ina wafuatiliaji wengi, wengi wao ni watu wenye asili ya Pwani ambao wanauchukulia wimbo huu kama sehemu ya utamaduni wakiuhusisha na ngoma yao ya asili Pungwe.

Wimbo wa msanii “Mdogo Mdogo” wa msanii mahiri hapa nchini, Diamond Platnumz, ndiyo uliofungua pazia la muziki wa Singeli.  Japo muziki huo si Singeli moja kwa moja ila una vionjo vya Singeli na wasanii wengi wa muziki huo wanautumia wimbo huo kama njia ya kuandaa nyimbo zao. Wimbo huu unapendwa sana Zanzibar na Mombasa kwa kuwa na mahusiano na ngoma ya asili Pungwe.

 Na Salum Milongo/GPL.