Cristiano Ronaldo na mpenzi wake Georgina Rodriguez mwenye kikoti cheusi.
MADRID, Hispania| Gazeti la Championi Ijumaa, Toleo la Jan. 06, 2016
STAA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anajulikana kwa kuwa ni mtu wa ‘totoz’, sifa hiyo alipewa kutokana na kawaida yake ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na wasichana wengi warembo.
Suala la kutajwa kufanya ngono au kuwa kwenye uhusiano wa muda mfupi na mrembo fulani maarufu hilo kwake siyo jambo geni.
Mrembo pekee ambaye alidumu naye kwenye uhusiano kwa muda mrefu ni Irina Shayk, mwanamitindo ambaye sasa ana umri wa miaka 30. Baada ya kutengana kwao mwaka jana, Ronaldo alikuwa kimya katika masuala ya kimapenzi huku ikiwa haijulikani ametulia kwa mrembo yupi baada ya hapo.
Baada ya kutulia kwa miezi kadhaa, mwishoni mwa mwaka jana, Ronaldo akaibuka na Georgina Rodriguez, mrembo wa Kihispania na kuwafanya watu waanze kuulizana juu ya msichana huyo.
Ronaldo na Georgina walianza kuonekana pamoja wiki kadhaa nyuma wakiwa kwenye matembezi katika maduka kadhaa, lakini safari hii alianza kwa siri tofauti na ilivyokuwa wakati anaanza na Irina ambapo waliweka wazi mambo yao mengi.
Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanamhusu Georgina na Ronaldo ambaye mwezi ujao anatarajiwa kutimiza umri wa miaka 32, wakati mpenzi wake huyo ana miaka 21:
WALIKUTANA KWENYE SHOO YA MAVAZI
Walianza kukutana kwenye sherehe jijini Madrid, mrembo huyo alikuwa akifanya kazi ya masuala ya mitindo, pia alikuwa ameajiriwa katika Duka la Gucci.
Wakati anakua, Georgina alijifunza masuala ya kudansi lakini baadaye akabadili na kuwa mwanamitindo.
ALIMTEMBEZA MIJI TOFAUTI
Baada ya kuelewana, Ronaldo alianza kutoka naye na kwenye sehemu mbalimbali zenye mikusanyiko ya watu huku mchezaji huyo akiwa anavaa mavazi yanayoficha uso wake kwa sehemu kubwa ili kukwepa usumbufu wa kujulikana.
Moja ya miji ambayo alimpeleka wakafurahia maisha ni Paris, Ufaransa ambapo walinaswa wakibusu na kuonyeshana mambo mengine ya kimahaba.
MAHABA YAMEMTULIZA RONALDO
Inaelezwa kuwa tangu waanze kuwa pamoja, kisaikolojia Ronaldo ametulia na kufanya mambo mengikatika mstari unaoeleweka, kiwango chake kimekuwa kizuri tofauti na mwanzoni mwa msimu alivyoanza.
Uwepo wa mrembo huyo uwanjani wakati Ronaldo akicheza umeongeza nguvu kwa kuwa mara k adha a
amewahi kupiga picha akiwa Bernabeu wakati Real Madrid inapocheza.
Ronaldo na mpenzi wake, Georgina wakiingia kwenye hoteli ya CR7 iliyopo Funchal, Madeira
UHUSIANO WAO ULIANZA ZAMANI KIDOGO
Kama ilivyoelezwa juu kuwa ulianza kwa siri, yawezekana Ronaldo maarufu kwa jina la CR7 alitaka kumsoma binti huyo kabla ya kufikia uamuzi wa kujionyesha naye hadharani.
Kuna picha kwenye Instagram zilizowekwa tangu Agosti mwaka jana zilithibitisha hilo, licha ya watu wengi kuanza kugundua mwishoni mwa mwaka jana.
GEORGINA ALIZALIWA JACA
Georgina ni mzaliwa wa Jaca, huu ni mji uliopo Kaskazini Mashariki mwa Hispania, ni mwendo wa saa nne kwa gari kutoka Jiji la Madrid.
Kuna kipindi aliwahi kuishi London na kujifunza Kingereza, alipomaliza mafunzo yake hakurejea Jaca badala yake akaenda Madrid na kuanza kujihusisha na masuala ya mitindo.
MAISHA BINAFSI YA RONALDO
Ronaldo ni baba wa mtoto mmoja, licha ya soka anafanya biashara mbalimbali ambazo zinasimamiwa na mama yake kwa kuwa baba yake, José Dinis Aveiro, alifariki akiwa na umri wa miaka 52 kutokana na unywaji wa pombe uliopitiliza.
Kutokana na kifo cha baba yake, Ronaldo aliapa kutokunywa pombe. Mama wa mtoto wake hajulikani mpaka leo kwa kuwa wakati anazaliwa Juni 7, 2010 hakukuwa na taarifa za mama mtu na mpaka leo hajawahi kusema chochote. Mtoto huyo anaitwa Cristianinho.
Ronaldo ni Mkristo wa madhehebu ya Katoliki, hana tatuu mwilini kwa kuwa amekuwa akichangia damu mara kadhaa.