Azam Fc wametinga fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuichapa Taifa Jang’ombe bao 1-0. Mfungaji wa bao hilo ni Frank Domayo mechi imepigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam wanasubiri mshindi kati ya Simba na Yanga ili wacheze naye fainali.