×

Mwanamke Achapwa Viboko Hadharani Mbele ya Rundo la Wanaume

vibokooKupitia mitandao ya kijamii imesambaa video ikionyesha kundi la wanaume wakishirikiana kumchapa viboko mwanamke mmoja ambaye hakufahamika mara moja alikosa nini.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi wala wizara yenye dhamana zinadai kuwa tukio hilo limetokea  Kijiji cha Nyasurura, Serengeti mkoani Mara.

Katika video inayosambaa mitandaoni, wanaonekana wanaume ambao wapo kwenye mkusanyiko kama vile mkutano huku wakiwa wameshika fimbo na kumchapa mwanamke huyo kwa zamu.

Wizara ya Afya, pamoja na Jeshi la Polisi tayari zimanza uchunguzi kufahamu kwanza kama tukio hilo limetokea nchini Tanzania, na kama ni Tanzania ni sehemu gani ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi.

Serikali imeviagiza vyombo vyake vya kiuchunguzi kufuatilia chanzo cha picha inayoonyesha mwanamke mmoja akichapwa viboko mbele ya mkutano.

Aidha vyombo vya dola vimetaiwa kufanya uchunguzi ndani ya muda mfupi na kutoa taarifa rasmi na Serikali haitasita kutoa adhabu kali kwa wote waliohusika.

Leave a Comment