
Alhaji Abdallah Bulembo akisalimiana na Rais John Magufuli.Picha ya Maktaba
DAR ES SALAAM: Rais John Pombe Magufuli, leo Januari 16, 2017 amewateua Prof. Palamagamba Kabudi na Alhaji Abdallah Bulembo kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa iliyoletwa na Kitengo cha Mawasiliano cha Ikulu leo, imeeleza kuwa wabunge hao wateule wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia, Rais Magufuli amemteua Benedicto Martin Mashiba kuwa Balozi.
Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Benedicto Martin Mashiba vitatangazwa baadaye.