×

Madereva Wakanusha Taarifa za Mgomo

aMwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWA), Shabani Mdemu (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

bMsemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Wema naye akizungumza jambo.

cMkutano na wanahabari ukiendelea.

MWENYEKITI wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWA), Shabani Mdemu leo amekanusha taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya mitandao ya kijamii hapa nchini kuwa madereva wamepanga kufanya mgomo Februari 26 mwaka huu akisema taarifa hizo si za kweli na madereva wanapaswa kuzipuuza.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mdemu amesema chama hicho hakijapanga mgomo wowote kama ilivyoripotiwa na mitandao ya kijamii hivyo wananchi wazipuuze taarifa hizo.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Wasafirishaji kwa Njia ya Barabara, Salum Abdallah alitoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa za kuwepo kwa mgomo wa madereva kama ilivyoripotiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii na kuliomba Jeshi la Polisi kuchukua hatua kwa wote waliohusika kusambaza taarifa hizo za upotoshaji.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam